TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 23, 2015

Dodoma wasisitiza ‘live’ Tamasha la Pasaka

index
Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa Mkoa wa Dodoma wametoa wito kwa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, kuweka mkazo kwa waimbaji watakaopanda jukwaani kwenye tamasha hilo mwaka huu ili kuendana na miaka 15.
Kwa mujibu wa Katibu wa Kwaya ya Mtakatifu Andrea ya mkoa ni humo, Wilson Hoya waimbaji wakiimba live kwenye Tamasha hilo itakwenda sambamba na miaka 15  ya tamasha hilo  la kumuabudu na Kumtukuza Mungu.
Hoya alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa waandaaji wa tamasha hilo kuukumbuka na kuuweka katika orodha ya mikoa itakayofikiwa na tamasha hilo mwaka huu.
“Mwishoni mwa mwaka jana, Kamati ilielekeza neno la Mungu katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea kwenye Tamasha la Krismasi, tunaomba Tamasha la Pasaka Dodoma iwepo kwenye orodha ya mikoa itakayopata upako kupitia tamasha la Krismasi,” alisema Hoya.
Hoya alisema Dodoma ni mkoa wenye fursa nyingi ambazo  zinapatikana kwenye Tamasha la Pasaka ambalo linasaidia maisha ya wakazi wengi wa mkoa huo.

No comments:

Post a Comment