TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 24, 2015

Rais Kikwete kupokea vitabu Milioni 2.5 vua shule za Sekondari nchini

HAPPY SHIRIMA – MAELEZO index
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete leo tarehe (24/02/2015) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye makabidhiano ya vitabu Milioni 2.5 kutoka Serikali ya Marekani kwa ajili ya shule za sekondari za Serikali . Taarifa hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Jumanne Sagini ambapo amesema vitabu hivyo ni kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne. Aliongeza kwamba makabidhiano hayo yatafanyika katika shule ya Sekondari Mtakuja iliopo eneo la Kunduchi Jijini Dar es salaam, hivyo Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Msaada la Marekani (USAID) watatoa msaada wa vitabu hivyo. Makabidhiano hayo yatafanywa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe Mark Childress kwa niaba ya Watu wa Marekani ,ambapo atamkabidhi Rais Kikwete. Alisema vitabu hivyo vimepatikana kutokana na juhudi za Rais Kikwete katika kuhakikisha kwamba shule hizo zinakuwa na vitabu vya masomo ya hisabati na sayansi vya kutosha ili kuimarisha ufundishaji wa masomo hayo kwa shule za sekondari nchini . Aidha aliongeza kwamba msaada huo umetokana na ziara ya Rais Kikwete nchini Marekani ambapo Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama alikubali kuchapisha vitabu hivyo vya Fizikia 533,520, Bailojia 666,480 , Hisabati 766,480 na Kemia 533,520 kwa ajili ya ufundishaji wa masomo hayo kwa shule za sekondari hapa nchini. Hata hivyo Katibu Mkuu Sagini ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika hafla hiyo muhimu na ya kihistoria kwa nchi ya Tanzania kupokea msaada huo wa vitabu.

No comments:

Post a Comment