TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 25, 2015

Mkuu wa Idara ya utumishi wa umma Mpanda Bw. Peter Kijika aagwa

kata1
Picha ya pamoja wa kwanza aliyevaa shati jekundu ni Katibu wa TSD Mkoa wa Katavi Deogratias Shija ,wa pili ni aliyekuwa Katibu wa TSD Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Peter Kijika,watatu ni Bi Debora Mwakaje Afisa Utumishi wa TSD,aliyevaa shati jeupe ni Alphonce Mwakyusa Afisa Utumishi Kaimu Katibu TSD Halmashauri ya Mpanda.
kata2
…………………………………………………………………………………..
Na Kibada Kibada -Katavi
Watumishi wa Ofisi ya Rais ,Tume ya Utumishi wa Umma Idara ya Utumishi wa Walimu TSD Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imefanya hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo Bw Peter Kijika kwa kuitumikia Idara hiyo kwa utumishi uliotukuka.
Akizungumza akizungumza katika Hafla hiyo mgeni rasmi katika hafla hiyo Katibu (TSD) Mkoa wa Katavi Bw,Deogratias Shija alisema kwa niaba ya Tume ya Utumishi wa Umma  alimshukuru kwa kuitumika Idara kwa utumishi wake uliotukuka.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na watumishi kutoka Idara hiyo walishukuru kwa jinsi walivyoishi na kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Bw Kijika aliyemaliza muda wake wa utumishi kwa kuitumika serikali hadi kufikia kupata utumishi uliotukuka.
Hafla hiyo ya kumuaga aliyekuwa Katibu wa TSD Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Peter Kijika ilifanyika kwenye ukumbi wa Idara ya TSD Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Kwa upande wake Kijika aliwashukuru wafanyakazi waliokuwa wakishirikiana katika utendaji kazi,wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu katika kusuma mbele gurudumu la Maendeleo na kuwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa kwa kujituma na kujitoa kwa ajili ya kulitumika taifa hadi nao waweze kufanikiwa kufika hatua ya kustafu.
Waliohudhuria katika hafla hiyo ni Mgeni rasmi Deogratias Shija,Katibu wa TSD,Peter Kijika,Katibu Mstaafu TSD,Mpanda,Alphonce Mwakyusa,Afisa utumishi Katibu TSD Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.Debora Mwakaje Afisa utumishi TSD Mkoa,Linda Steveni Afisa utumishi Halmashauri ya Wilaya Mpanda,Rehema Kilembwa kaimu TSD  Halmashauri ya Mjini Mpanda,na Benson Ngamilo Kaimu Katibu TSD Halmashauri ya Nsimbo.
 

No comments:

Post a Comment