TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 23, 2015

HABARI ZILIZOTAWALA NA KUSOMWA ZAIDI SIKU YA JANA JUMAPILI TAREHE 22/2/2015

Rais Kikwete akagua vijiji vilivyoathiriwa na Mvua Chalinze

7
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwasili kwa helikopta katika kata ya Chalinze wakitokea jijini Dar es Salaam jana, kukagua uharibifu ulioletwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kuharibu makazi ya watu na kujeruhi ambapo kaya 47 zikiathirika katika vijiji vya Msoga na Tonga.
(picha zote na Freddy Maro)
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa kata Ya Chalinze wakikagua baadhi ya nyumba zilzoharibiwa vibaya baada ya kuangukiwa na miti kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika kata ya Chalinze na kuathiri kaya 47.Rais Kikwete alikagua uharibifu huo, kuzungumza na kuwafariji wana vijiji hao na kuahidi kuwasaidia katika janga hilo

3
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakizungumza na wana vijiji waliopatwa na dhoruba la mvua.
45
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wana vijiji hao na kuahidi kuwasaidia katika janga hilo

…………………………………………………………………………
  Na Freddy Maro Chalinze,Bagamoyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana aliwafariji na kuahidi kuzisaidia kaya 40 ambazo nyumba zao ziliharibiwa vibaya na mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki iliyopita huko Chalinze,wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Katika ziara hiyo Rais Kikwete ambaye alikuwa amefuatana na mkewe mama Salma Kikwete alikagua Shule ya msingi Chalinze, Ofisi ya CCM, na nyumba kadhaa za wanakijiji ambazo ziliharibiwa vibaya na mvua hizo na kujeruhi baadhi ya wanavijiji walioangukiwa na nyumba zao.
“Nimepata taarifa ya maafa yaliyotokea, sikuwepo kwahiyo nimekuja kuwapa pole.Poleni sana Kwa wale ambao nyumba zimeharibika serikali inao utaratibu wa kusaidia.Mkurugenzi akipata taarifa atajua jinsi gani ya kuwasaidia.Lakini kuna misaada tunayoweza kutoa.Nasikia Mbunge ametoa msaada wa chakula na dawa pamoja na matibabu.Lakini Kwenye serikali tunao wajibu wetu.Mkurugenzi yupo taarifa zipilekwe kwake kwa uhakika ilitujue la kufanya.Poleni sana tutaendelea kusaidiana,” alisema Rais Kikwete ambaye pia ni Mkazi wa kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze.
Mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki liyopita iliharibu kabisa majengo nane katika kata ya Chalinze ambapo kuta zilibomoka mabati kuezuliwa na upepo mkali na miti kuangukia nyumba na kujeruhi wana kijiji kadhaa ambao walitibiwa katika hospitali ya Tumbi.Kaya 47 kutoka vijiji vya Msoga na Tonga ziliathirika na mkasa huo.

 

YANGA YAICHAPA MBEYA CITY 3-1

MRISHO-NGASSA
VINARA wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, Leo huko Sokoine, Jijini Mbeya wamepaa kileleni wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili na Mabingwa Watetezi, Azam FC, baada ya kuichapa Mbeya City Bao 3-1.
Bao za Yanga hii Leo zilifungwa na Simon Msuva, Mrisho Ngassa na Amisi Tambwe wakati lile la Mbeya City lilipachikwa na Peter Mapunda.
Katika Mechi nyingine ya Ligi iliyochezwa Leo huko Kambarage, Stand United waliitungua Simba Bao 1-0.
Mechi ya mwisho hii Leo itachezwa Usiku huu huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kati ya Azam FC na Tanzania Prisons.

MKURUGENZI ALEX MSAMA AMWAGA MISAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA, ALAANI MAUAJI YA ALBINO YANAYOENDELEA NCHINI

1Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Halima Ramadhan Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwadaliwa kilichopo Tegeta jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni moja ya misaada inayotolewa katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima wakati wa msimu huu wa maadalizi ya Tamasha la Pasaka linalotimiza miaka 15 tangu lianzishwe.
Tamasha hilo Litafanyika  jijini Dar es salaam Aprili 7  2015 na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa kimataifa na waimbaji wa ndani, Katika Tamasha hilo pia kutakuwa na michezo mbalimbali itakayochezwa ikiwa ni pamoja na kukabidhi zawadi na vikombe kwa washiriki wa Tamasha hilo, Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo zilizoko Kinondoni jijini Dar es salaam.
Alex Msama amelaani mauaji ya Albino na kuiomba serikali kuweka mkazo katika kushughulikia wahalifu wanaofanya ukatili huu na kuua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), ili kukomesha mauaji hayo hapa nchini ambayo yanalitia aibu taifa 2Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Honorata Michael  Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Honorata kilichopo Temeke jijini Dar es salaam. 3Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Rashid Mpinda  Katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni Mosco jijini Dar es Sakaam. 4Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Soud Said  Mwakilishi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Ijanzo Zanda orphanage Centre cha jijini Dar es salaam 5Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Hadija Mwambungu kutoka kituo cha  kulelea watoto yatima cha Malaika Kids kilichopo Mwananyamala Mwinjuma jijini Dar es salaam. 6Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akiakihelezea zaidi kwa waandishi wa habari juu ya misaada hiyo iliyotolewa na kampuni yake kwa vituo hivyo wakati huu wa maandalizi ya tamasha la Pasaka. 7Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Bw Hudson Kamoga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya tamasha la pasaka. 8Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akiakiwa amewabeba baadhi ya watoto wa kituo cha Honorata wakati alipowakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali. 9Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akihojiwa na mwaandishi wa habari wa BBC Bw. Anold Kayanda mara baada ya kukabidhi misaana hiyo ambapo aliiomba serikali kuweka mkazo katika kushughulikia wahalifu wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino)ili kukomesha mauaji hayo hapa nchini

JE UMEFUNGUA/UNATAKA KUFUNGUA KAMPUNI, JIFUNZE KAMPUNI YAKO INAVYOTAKIWA KULIPA KODI KISHERIA.

images 
Na Bashir Yakub
Vijana wengi wajasiriamali wadogo wamefungua makampuni. Hakika wote waliofanya hivi wamefanya jambo jema linaloendana na wakati. Niliwahi kuandika wakati nikielekeza namna nyepesi kabisa ya kufungua kampuni kuwa, ni vigumu kwa leo kufanya biashara na ukawa na mafanikio nje ya kampuni. Nikasema hata kama unauza maziwa, mama ntilie, unauza mayai, kibanda cha huduma ya fedha kupitia simu,unauza mihogo, haizuiwi kufungua kampuni. Kuna kampuni hata za mtaji wa milioni moja na pesa hiyo si lazima uwe nayo mkononi ila ni katika maandishi tu. Nikasema anayetaka mafanikio kwa sasa ahakikishe hiyo biashara yake ndogo kabisa anaifungulia kampuni. Kwakuwa wapo wengi ambao tayari wamefungua makampuni basi zipo changamoto nyingi wanazokumbana nazo na kubwa zaidi ni taarifa au ujuzi wa mambo mbalimbali ya namna ya kuendesha kampuni ili kampuni iwe kampuni kweli. Moja ya eneo lenye shida au ambalo wajasiriamali wadogo hawana taarifa nzuri kuhusu ni taarifa za kodi zinavyolipwa na kampuni kisheria. Hawajui ni kiasi gani, kwa muda gani na vipi. Leo hapa nitaeleza kwa uchache kuhusu kodi za kampuni. Kampuni hulipa kodi ya mapato, swali ni kodi ya mapato nini.
1. KAMPUNI HULIPA KODI YA MAPATO, JE KODI YA MAPATO NINI ?
Kodi ya mapato Tanzania ni tozo kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na vyanzo vitatu ambavyo ni ajira, biashara pamoja na uwekezaji. Aina hii ya kodi inatozwa kwa mamlaka ya Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, kama ilivyorekebishwa.Kwa upande wetu wa kampuni kodi inayolipwa kwa tafsiri hiyo hapo juu ni kwakuwa kampuni ni biashara na pia ni kwakuwa ndani kampuni waweza kuwamo uwekezaji.Hii ndio sababu kampuni hulipa kodi ya mapato.
2. JE WAJUA KUWA SI KILA KAMPUNI HUTAKIWA KULIPA YA MAPATO.
Mjasiriamali anatakiwa kujua kuwa si kampuni zote hutakiwa kulipa kodi ya mapato. Kampuni zinazotakiwa kulipa kodi ya mapato ni kampuni zenye Dhima ya ukomo. Kampuni zenye dhima ya ukomo ni zile zote ambazo ni Limited. Kama kampuni yako ni Limited (LTD) basi inatakiwa kulipa kodi ya mapato. Nyingine zinazotakiwa kulipa kodi ni kampuni za kudumu za ndani na matawi ya Kampuni za wageni/wasio wakazi. Hizi hazihusiki na wajasiriamali sitazifafanua zaidi.
Aidha,kama kampuni umeiunda na umeingia ubia na kampuni nyingine basi hutakiwi kulipa kodi ya mapato.
3. USIOGOPE KODI HUTOZWA KATIKA FAIDA TU NA SI KUTOKA KILA FEDHA UNAYOINGIZA.
Kodi ya mapato ya kampuni hutozwa kwenye faida tu iliyotokana na shughuli za biashara za kampuni au faida uliyoipata kutokana na uwekezaji. Umeunda kampuni umempata mtu ana mtaji akawekeza mtaji, faida inayopatikana hapo ndiyo faida kutoka katika uwekezaji. Ifahamike kuwa si kweli kuwa kila unachoingiza lazima kilipe kodi.
Continue reading →

MKAKATI WA KUENDELEZA ENEO LA MAPOROMOKO YA MTO KALAMBO MKOANI RUKWA WACHUKUA SURA MPYA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa baadhi ya maelekezo kwa fundi anaejenga geti litakalotumika kutoza ushuru kwa watalii wa nje na wa ndani watakaofika kuona maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls) ambayo ni maporomoko ya pili kwa ukubwa barani Afrika. Maporomoko hayo ambayo yapo Mkoani Rukwa mpakani na nchi jirani ya Zambia yamekuwa yakinufaisha zaidi upande Zambia ambao wamejenga miundombinu kadhaa kuwawezesha na kuwavutia wanaofika kuona maporomoko hayo. Mto unaotengeneza maporomoko hayo upo nchini Tanzania na hata muoenekano mzuri unapatikana kutokea upande wa Tanzania. Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ameamua kusimamia kidete kuhakikisha miundombinu kadhaa inajengwa katika eneo hilo la maporomoko ili rasilimali hiyo adimu iweze kutambulilaka na kutoa mchango wa kiuchumi kwa taifa na Halmashauri husika ya Wilaya ya Kalambo.
Jengo ambalo litatumika kama geti la kuingilia katika maporomoko ya Mto Kalambo na ambalo pia litatumika kama eneo la kutoza ushuru kabla ya watalii kuingia kushuhudia maporomoko hayo likiwa katika hatua ya ujenzi wa awali.
 Afisa Habari Mkoa wa Rukwa Ndugu Hamza Temba akifurahia maajabu ya maporomoko ya Mto Kalambo.
 Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Frank Maten(Kulia) na baadhi ya watalii wa ndani waliofika kuangalia maporomoko hayo wakifurahia maumbile ya asili ya eneo hilo.
Picha ya pamoja.
(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

UVCCM MKOA WA LINDI WALAANI MAUAJI YA ALBINO NA KUMPONGEZA RAIS KWA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA.

DSCF6604
Baraza Kuu la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Lindi chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Amir M. Mkalipa, wamefanya kikao cha kikanuni leo tarehe 21 Feb. 2018, katika ukumbi wa mikutano wa ofisi kuu ya CCM Mkoa wa Lindi, iliyopo Wailes, Lindi mjini.
Pamoja na kujadili hoja zingine zinazohusu uimara wa jumuiya mkoani Lindi, changamoto za Vijana na Walimu, suala la migomo ya wafanyabiashara, na kuwataka watendaji wa Serikali kutimiza wajibu na majukumu yao kikamilifu ili kuongeza ufanisi wa Serikali katika kutatua kero za wananchi na kuleta maendeleo ya jamii, lakini pia kikao hicho kimeazimia:-
a} Baraza kuu la UVCCM Mkoa wa Lindi imeitaka Serikali kuendelea kuchukua hatua kali kwa watakaobainika kuhusika na mauaji ya Albino. Ni lazima Serikali kushirikiana na wananchi wahakikishe ndugu zetu Albino wanaishi maisha yenye usalama, amani na furaha kwani ni haki yao kikatiba.
b}Pia, Baraza Kuu la UVCCM Mkoa wa Lindi linampongeza Mhe. Rais na Mwenyekiti wa CCM ndugu Jakaya Kikwete kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM (2010-2015) kwa kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kibiti-Mingoyo,
Pia inampongeza Mhe Rais Jakaya Kikwete kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Lakini pia, UVCCM inampongeza na kumuunga mkono Mhe Rais kwa uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 27 ambapo baadhi ya wateule hao wanatoka kwenye jumuiya hiyo, jambo ambalo ni heshima kubwa kwa UVCCM, na kudhihirisha kuwa jumuiya hiyo inatimiza wajibu wake wa kuwa tanuru la kuoka viongozi wenye uwezo, waadilifu na wenye kuaminika katika jamii. Pia UVCCM imewapongeza ndugu Mboni Mhita na ndugu Paul Makonda kwa kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na kuwataka wakatimize wajibu kwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na ufanisi.
Pia, UVCCM Lindi inampongeza Kamanda wa Vijana Mkoa Mhe Bernard Membe-Mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kwa kuwa karibu na Vijana na kuiwezesha jumuiya kutimiza majukumu yake.
C} Mwisho, UVCCM Mkoa wa Lindi inahimiza Halmashauri za wilaya kutenga asilimia 10% ya Mapato yake kwa ajili ya maendeleo ya Vijana na Wanawake, ili vijana wanufaike kwa mikopo na waweze kujiajiri ili kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini. Jambo hili lipo kisheria sio ombi, hivyo watendaji husika wa Serikali wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo ama UVCCM itawalazimisha kutimiza wajibu huo.
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi, wamepitisha ratiba ya shughuli zao kwa Mwaka 2015 na wataanza ziara ya kutembelea Vijana katika wilaya zote sita (6) za Mkoa wa Lindi.

Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein afungua Madrasatul Al-Tawheed wilaya ya kusini unguja

unnamed
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuifungua  Madrasatul Al-Tawheed iliyopo Kiongoni Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja jana alipofanya ziara maalum katika wilaya hiyo (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mhe,Haroun Ali Suleiman,
[Picha na Ikulu.]

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ampa pole Chief wa Wahehe , Adam Abdu Sapi Mkwakwa

1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Chief wa Wahehe , Adam Abdu Sapi Mkwakwa   wakati alipokwenda nyumbani kwa Chief huyo, Kalenga Iringa  Februari 20, 2015 baba yake Chief huyo, Marehemu Abdu Adam Sapi Mkwawa uliotokea hivi karibuni.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
2
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishiriki katika dua mbele ya kaburi la marehemu Abdu Adam Sapi Mkwawa   wakati alipokwenda nyumbani kwa Chief huyo, Kalenga Iringa   kuhani.
6
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizunbgumza na viongozi wa wilaya ya Kilolo baada ya kusomewa taarifa ya wilaya hiyo Februari 21, 2015. Kushoto ni Mkuu wa koa wa Iringa, Amina Masenza.
7
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na mkewe Tunu  wakisalimiana na walimu  wa sekondari ya Ilula kabla ya kukagua ujenzi wa maabara katika shule hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa.
8
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua moja ya madara ambayo yamegeuzwa kuwa maabara katika Shule ya Sekondari ya Ilula akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 21, 2015. Kitendo hicho hakikumfurahisha na aliagiza kisirudiwe tena sehemu nyingine ngo mapya yajengwe kwa ajili ya maabara
9
Mke wa Waziri Mkiuu, Mama Tunu Pinda akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilulawilayani Kilolo ambako Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alikagua ujernzi  wa maabara na kuhutubia wananchi. 
10
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua banio katika mradi wa umwagiliaji maji wa kijiji cha  Nyanzwawilayani Kilolo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 21, 2015.
12
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakikagua shmba la vitunguu la Bw. Furaha Ngalali  (kulia)  wakati walipotembelea mradi wa umwagiliaji wa kijiji cha Nyanzwa wilayani  Kilolo Februari 21, 2015.
13
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na   Meneja Mipango wa Kamouni ya Mawasiliano ya simu ya VIETTEL TANZANIA LIMITED tawi la Iringa, Salvatory Elikidus katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkiuu, Mizengo Pinda katika kijiji Nyanzwa wilayani Kilolo Februari 21, 20154.  Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Tawi la Iringa,  Tran  Nhat Duy na wapili kushoto ni  Mkuu wa Idara ya Fedha, Vo Ngoc Thang.

CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI CHATOA TAMKO KUHUSU SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 ILIYOZINDULIWA NA RAIS JAKAYA KIKWETE FEBRUARI 13, 2015

 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Zanzibar, Musa Kombo Musa (kulia), akimkaribisha Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia (katikati), ili azungumze na wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitoa tamko hilo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosene Nyambabe.
 Mwenyekiti  wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Taifa, James Mbatia (kulia), akionesha kitabu cha Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa tamko la chama hicho juu sera hiyo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosene Nyambabe na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Musa Kombo Musa.
 Hapa mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
Wajumbe wa Halmshauri Kuu (NEC) ya chama hicho waliokuwepo kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Honest Mombory, Katibu wa Wazee, Ernest Mwasada, Dk.Nderakindo Kessy ambaye pia pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Angelina Mutahiwa na Esther Komba.
…………………………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia amesema kuwa uzinduzi wa Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 ni mpango wa serikali kuwalaghai wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba mwaka huu.
Pia amesema hali ya elimu nchini ni kama mgonjwa aliyekuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, hivyo serikali isiwe inatoa majibu mepesi kwenye masuala magumu ambayo yanagusa maisha ya watanzania.
Akizungumza Dar es Salaam leo wakati akitoa tamko la chama hicho kuhusu sera hiyo Mbatia  alisema kuwa mnamo Januari 31 na Februari mosi mwaka 2013, aliwasilisha hoja bungeni kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu.
Alisema kuwa aliorodhesha athari mbalimbali za udhaifu wa wa elimu itolewayo nchini lakini suala hilo lilionekana kutawaliwa na siasa ambapo haikuwa lengo lake,lengo lilikuwa kuhakikisha kuwa sera mbalimbazi za elimu zinaboreshwa.
Mbatia aliongeza kuwa mnamo Februari 13, 2015 mwaka huu Rais Jakaya Kikwete, alizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 lakini ikiwa haijajibu hoja alizokuwa amezitoa.

Alifafanua kuwa wakati Rais akihutubia alisema kuwa sera hiyo ilitumia miaka saba kukamilika, lakini Mwenyekiti huyo alisema baada ya kuipitia alibaini sera hiyo kuwa na lugha ngumu huku ikiwa na makosa mengine mengi.
Mbatia alisema anachokiona kwa serikali kuzindua sera hiyo mwaka huu ni mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu,kwani yaliyomo ndani ya sera hiyo yamelenga kuwalaghai wapiga kura.
Aidha alisema mambo hayo ni pamoja na kutangaza kuwa elimu ya msingi kutolewa bure bila karo na lugha iliyotumika inawachanganya watanzania hivyo ni vigumu kwa wananchi wa vijijini ambao wengi wao hawana elimu kutambua yaliyoandikwa ndani ya sera hiyo.
“Mfano sera mpya ina matamko mawili ambayo  inawachanganya watanzania kuhusu lugha ya kufundishia,moja inatamka Kiswahili kitatumika kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu,na ya pili inatamka kuwa Kingereza kitatumka kama lugha ya kufundishia katikan ngazi zote za elimu.
“Matamko haya mawili, kwanza yanakwepa lawama zinazotokana na malumbano ya muda mrefu kuhusiana na lugha gani inafaa kufundishia, pili imehalalisha mifumo miwili ya elimu ndani ya nchi moja” alisema Mbatia kwa msisitizo 
Hivyo alisema serikali ilipaswa kutengeneza sera ambayo inazungumza kwa uhakika kuhusu suala la lugha ya kufundishia, kuliko kutoa tamko la sera lisilo na msimamo.
Aliweka wazi kuwa wanapendekeza iundwe tume ya kudumu ya elimu nchini itakayoshughulikia pamoja na mambo mengine kuhakikisha ubora wa elimu unapatikana nchini.
Vilevile alisema wanaiomba serikali kupitia upya sera hiyo kabla haijaanza kutumika ili kuepusha taifa na madhara ambayo yameonesha dalili za kutokea hata kabla haijaanza kutumiaka. (Imeandaiwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

DRFA,YAMLILIA KIUNGO WA ZAMANI WA SIMBA NA TAIFA STARS-CHRISTOPHER ALEX

Christopher Alex 
Chama cha kandanda mkoa wa Dar es salaam DRFA,kimeeleza kusikitishwa kwake na kifo cha mchezaji kiungo wa zamani wa klabu ya simba na timu ya taifa-Taifa Stars,Christopher Alex  maarufu kama Masawe,kilichotokea leo (februari 22 mwaka huu),katika Hospitali ya MirembeDodoma.
Mwenyekiti wa DRFA,Almas Kasongo,amemuelezea marehemu Christopher kuwa ni mchezaji aliyevuma enzi za uhai wake na kuiletea heshima kubwa klabu yake ya Simba na Taifa Kwa ujumla,pale walipofanikiwa kuisukumiza nje ya michuano ya afrika klabu ya Zamalek na kuivua ubingwa miamba hiyo ya soka ya kaskazini mwaka 2003.
Kiungo huyo aliyeanza kuvuma katika miaka ya 2000,amefariki dunia kutokana na kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua kikuu (TB).
Marehemu Christopher Alex, alizaliwa Septemba 12 mwaka 1975,na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Uhuru na kumaliza katika shule ya Chamwino huko Dodoma mwaka 1993,na alianza kucheza mpira kwenye timu ya Daraja la nne Chamwino UTD na baadaye daraja la tatu akiwa na kikosi cha Aston Villa nayo ya Dodoma.
Mwaka 1999-2001 ameitumikia klabu ya CDA ya Dodoma,kabla ya kutimkia klabu ya Reli mwaka 2002 na baadaye kujiunga na wekundu wa msimbazi Simba,Marehemu ameacha mtoto mmoja aitwaye Alex.
Kasongo,kwa niaba ya kamati ya utendaji ya DRFA,wametoa ubani wa shilingi laki mbili (200,000/=) kwa familia ya marehemu,na kuwataka mashabiki wa soka na watanzania kwa ujumla kuungana pamoja katika kuifariji familia hiyo kwenye kipindi hiki kigumu cha majonzi.

WAZIRI MKUU: ANZISHENI HALMASHAURI NYINGINE KILOLO

indexWAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa mkoa wa Iringa uangalie uwezekano wa kuanzisha Halmashauri mpya katika wilaya ya Kilolo kata ya Mahenge na tarafa ya Mahenge kwa sababu ya hali ya kijiografia ya eneo hilo.
“Makao makuu ya wilaya hii yako Kilolo kule milimani. Ukitaka kuja huku ni lazima upite kwanza mjini ndipo ufike huku. Hapana! Hatuwezi kuwasaidia wananchi hawa kujiletea maendeleo kwa staili hii,” alisema Waziri Mkuu.
Alikuwa akihutubia wakazi wa vijiji vya Nyanzwa na Igunda wilayani Kilolo, jana jioni (Jumamosi, Februari 21, 2015) mara baada ya kukagua mradi wa umwagiliaji wa Nyanzwa ambao ni maarufu kwa kilimo cha vitunguu. Vijiji hivyo viko umbali wa km. 120 kutoka Ipogoro ilipo njia panda ya kwenda Iringa mjini na km. 155 kutoka Kilolo mjini yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.
Waziri Mkuu alisema kata za tarafa hiyo ni kubwa mno kwa mtendaji kuweza kusukuma maendeleo ya wananchi. “Kata hii imeanzia Kitonga hadi huku Nyanzwa. Hivi ni mtendaji gani anayeweza kuja kuhimiza shughuli za maendeleo akitokea huko?” alihoji Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
Alisema mbali na idadi ya watu, suala la kijiografia huwa linaangaliwa wakati wa kuanzisha maeneo ya utawala. “Hili eneo ni zuri, fursa zipo lakini linakosa usimamizi ndiyo maana hata wilaya hii inaongoza kwa umaskini kuliko wilaya nyingine za mkoa huu. Acheni wilaya ibaki moja, mbunge abaki mmoja lakini Halmashauri ziwe mbili ili muweze kusukuma maendeleo ya eneo hili kwa sababu mtakuwa na madiwani wenu na bajeti yenu,” alisema.
Mapema, akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mtendaji wa Kijiji cha Nyanzwa, Bw. Hekima Masanula Katemo alisema skimu ya umwagiliaji ya Nyanzwa ilijengwa mwaka 1960 wakati huo kwa kutumia banio la miti na magunia ya mchanga. Ilikuja kuboreshwa miaka ya 90 kwa ufadhili kutoka Jumuiya ya Ulaya na Serikali ya Sweden.
“Hata hivyo, skimu hii ambayo inahudumia wakulima 3,469 wakiwemo wanaume 1,662 na wanawake 1,807; inakabiliwa na uhaba wa maji kwani ni hekta 256 tu ambazo zinamwagiliwa kwa sasa wakati eneo lote la mradi ni hekta 940,” alisema Bw. Masanula.
Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake mkoani Iringa kwa kutembelea Manispaa ya Iringa ambako atakagua ujenzi wa maabara kwenye shule ya sekondari Kihesa, kuzindua kituo cha polisi cha Semtema, na kukagua huduma za afya kwenye hospitali ya manispaa ya iringa. Pia atakagua mradi wa machinjio ya kisasa ya Ngelewela kabla ya kutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja wa shule ya msingi Ipogolo.

 MKUTANO WA 16 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI NAIROBI,KENYA, KATIKA PICHA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Pierre Nkurunzinza wa
Burundi jijini Nairobi kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa kawaida wa
wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimwindikiza na Rais Pierre Nkurunzinza wa
Burundi walipokutana jijini Nairobi kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa
kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakipigiwa wimbo wa taifa wa
Tanzania baada ya kuwasili  kwenye ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa kawaida wa
wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015. Kulia ni Naibu
Rais wa kenya Mhe. William Samoei
Ruto
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wakisimama kwa wimbo wa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki   kwenye ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa 16
wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wakiwa meza kuu  kwenye
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiongoza  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akipeana mikono na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada
ya kupokea kijiti cha kuongoza jumuiya hiyo wakati wa   mkutano
wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania ambaye pia
ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya hiyo Dkt Harrison
Mwakyembe akiwasilisha ripoti ya mwaka ya baraza hilo   mkutano
wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Bango la wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Waziri wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri
wa Jumuiya baada ya kukabidhiwa  ripoti ya mwaka ya baraza hilo
mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akimuaga Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyekwemnda
kumuomba udhuru ili kuondoka mapema kabla ya kumalizika kwa
mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Jaji Geoffrey W. M. Kiryabwire akiongozwa kuelekea jukwaani kula kiapo kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete  akimpongeza Jaji Audace Ngiye kutoka Burundi
baada ya kula  kiapo  kuwa Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi
za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete  akimpongeza Mhe Liberag Mpfumukeko kutoka Burundi
baada ya kuteuliwa kuwa Nibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mshariki
wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki February 20, 2015
Waziri wa Ushirikiano wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki wa
Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya
hiyo Dkt Harrison Mwakyembe akishauriana jambo na  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika MasharikiJoyce
Mapunjo 
wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Wanafunzi washindi wa Insha wakisubiri kupokea tuzo zao katika
mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akipungia mkono wajumbe walioko Kampala baada ya Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya moja kwa moja kwa njia ya video uitwao Telepresence katika  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Ujumbe wa Tanzania katika  mkutano wa 16 wa kawaida wa
wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015, Kutoka kushoto ni
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mhe Bernard Membe, WAZIRI wa nchi
ofisi ya rais anayeshughulikian utawala bora Mhe. 
George Huruma Mkuchika,Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe  George Mcheche Masaju, Waziri wa Fedha, Mhe, Saada Mkuya Salum na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Lazaro Nyalandu
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akihutubia katika kilele cha   mkutano wa 16 wa
kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20,
2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa kenya na
Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini baada ya  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa kenya, Rais Pierre
Nkurunzinza wa Burundi na Naibu Rais wa kenya Mhe. William Samoei Ruto  baada ya mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015. Picha zote na IKULU

MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA UTALII ZANZIBAR (ZATI) WAFANYIKA MJINI UNGUJA.

mku1Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) Bi. Pamela Mattheuu (aliesimama) akielezea hali ya Utalii ilivyo kwa sasa na kupanga mikakati ya kuitangaza zaidi sekta hiyo, huko Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
mku2Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar Nd. Abdulsamad Said akizungumza na wanachama kuhusu mafanikio na changamoto zinazokabil sekta ya Utalii nchini katika Mkutano Mkuu uliofanyika Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar. mku3Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) akifungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) katika Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar). mku4Baadhi ya wanachama wa Jumuiya hiyo wakimsikiliza mgeni rasmin Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) kayupo pichani alipokuwa akifungua mkutano huo. mku5Mmoja wa wanachama wa ZATI Simai Mohamed Saidi akiuliza suali katika Mkutano huo uliofanyika Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
mku6 
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) wakatikati katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya (ZATI) Abdulsamad Said (kulia) na kushoto Makamu wake mstaafu Boby Mckena. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

Wanafunzi wa Chuo cha Taifa CHA UTALII WATEMBELEA TBL

 Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL),Castor Massawe (mbele katikati) jinsimalighafi za nafaka zinavyohifadhiwa katika ghala, walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam juzi.
 Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Castor Massawe (katikati) akitoa maelezo kuhusu upishi wa bia kwa njia ya kompyuta wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam juzi.
 Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Castor Massawe (katikati) akitoa maelezo kuhusu uchachuaji wa bia kwa njia ya kisasa wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam
 Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Castor Massawe (katikati) akitoa maelezo kuhusu uchachuaji wa bia kwa njia ya kisasa wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam
 Mhandisi Uzalishaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Castor Massawe (katikati) akitoa maelezo kuhusu uchujaji wa bia kwa njia ya kisasa wakati wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii walipotembelea kiwanda cha TBL, Dar es Salaam
Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, wakitembelea Kiwanda cha Bia Tanzania cha Dar es Salaam juzi, ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.

No comments:

Post a Comment