TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 25, 2015

MGOGORO WA MWEKEZAJI NA WANANCHI KUHUSU SHAMBA LA MAKANGALE WAMALIZIKA

images
Na Masanja Mabula -Pemba . Mgogoro wa shamba kati ya Mwekezaji  na wananchi wa Shehia ya Makangale umemalizika ambapo  pande hizo zimefikia makubaliano na kuahidi kushirikiana  kulinda na kudumisha amani pamoja na kukuza kipato chao kupitia sekta ya Utalii .
Makubaliano hayo yamefikiwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ambapo Mwekezaji Amit Ladwa amekubali kulipa fidia ya miti aina ya mivinje ambayo imepandwa na wananchi katika shamba hilo .
Akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika kwenye ufukwe wa Vumawimbi liliko shamba  , Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman ameiagiza Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka Pemba kuharakisha kufanya tathmini na miti hiyo ili wananchi walipwe fidia na Mradi huo uanze kutekelezwa .

Amesema kuwa ni jukumu la Idara hiyo kuhakikisha kwamba inavifanyia tathmini vitu vyote vilivyomo katika shamba hilo haraka iwezekanavyo ili mwekezaji alipe fidia inayostahili kwa wananchi jambo ambalo litatoa fursa kwa ujenzi wa hoteli .
“Leo hii tumeshughudia makubaliano yakifikiwa hapa , kilichobaki ni kwa Idara ya Misitu na Maliasili zisizorejesheka kufanya tathmini ya vitu vyote vilivyomo ndani ya shamba hili ili mwekezaji aweze kuwalipa wananchi fidia zao na ujenzi wa mradi uanze kutekelezwa ” alisisitiza Mkuu wa Mkoa .
Aidha Mkuu  huyo wa Mkoa amewataka wananchi wa shehia hiyo kumpa ushirikiano wa kila hali mwekezaji huyo wakati wote wa utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na ulinzi wa mali zake .
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Jabu Khamis Mbwana amefahamisha kwamba makubaliano hayo yamefikiwa kutokana na wananchi wa shehia hiyo kutambua umuhimu na faida za sekta ya Utalii katika kukuza uchumi wao na Taifa kwa Ujumla .
Amesema kuwa kufikiwa kwa makubaliano hayo ni ishara ya kuwepo na amani katika shehia hiyo na kuwataka wananchi kumpokea mwekezaji huyo na kisha kushirikiana naye ili aweze kusaidia klutatua baahi ya kero za kijamii .
“Makubaliano haya yamefikiwa kutokana na wananchi wa shehia hii kutambua umuhimu na faida ya Sekta ya Utalii katika kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla lakini nawaomba wananchi mpokeeni huyu mwekezaji  na shirikianeni naye ” alitilia mkazo Mkuu wa Wilaya .
 Awali wananchi hao wameitaka Serikali kutokuwa na hofu juu ya usalama wa mwekezaji huyo na kwamba watashirikiana naye kuanzia mwanzo hadi mwisho wa utekelezaji wa mradi huo .
“Kwa hili tunaiomba Serikali kuondoa hofu juu ya usalama wa maisha ya mwekezaji pamoja na mali zake sisi tupo pamoja naye na tutashirikiana  muda wote wa utekelezaji wa mradi huu ” alisema Kombo Ali Kombo kwa niaba ya wananchi wenzake .
Kwa Upande  wake mwekezaji Amit Ladwa ameelezea kwamba kipaombele cha kwanza cha ajira atakitoa kwa wakaazi wa shehia hiyo na kuongeza kwamba atatoa mafunzo ya lugha mbali mbali kwa vijana watakaokuwa tayari kufanya kazi hoteli hiyo ..
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ametembelea maeneo ambayo yanamigogoro ya ardhi likiwemo shamba la  Mzee Ali Said Ramadhaman (80) ambalo linadaiwa kupimwa bila ya mwenyewe kushirikishwa na kisha kukabidhiwa Samiya Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment