TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 24, 2015

PSPTB YAFANYA SEMINA YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WA BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi PSPTB imeendesha mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya shahada ya
Ununuzi na ugavi.
Mafunzo hayo yalifunguliwa tarehe 16 Februari 2015 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha, ambaye aliwaasa wanafunzi hao wazingatie mafunzo hayo ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti watakazofanya kwa ajili ya kupata shahada ya juu ya ununuzi na ugavi. Aidha, alisisitiza kuwa wanapaswa kuzingatia maadili katika kufanya utafiti, jambo ambalo ndio msingi na matakwa ya Bodi. wanafunzi wanatakiwa kufanya utafiti wao wenyewe na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine maana kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya utafiti, pia wanafunzi wanajengewa uwezo wa kujiamini, kuandika ripoti na kujieleza na hata kuwasilisha ripoti katika sehemu zao za kazi. Hivyo lengo kuu la semina hii ni kuwajengea uwezo wa kuandika, kujieleza na kutoa huduma bora kwa taifa, kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.
New Picture (88) 
Mr. Godfred Mbanyi, Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB akitoa neno katika ufunguzi wa semina ya utafiti iliyofanyika kwenye ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe 16/2/2015
New Picture (89)
Mkurugenzi wa mafunzo Mr. Godfred Mbanyi akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence TEsha kufungua semina ya utafiti katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam. Tarehe 16/02/2015

New Picture (90) 
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB na washiriki wa semina ya Utafiti iliyofanyika Katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe. 16/2/2015.
New Picture (91)Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence Tesha(aliyeketi katikati), mwezeshaji wa semina Dr. Eli Tumsifu (aliyeketi kushoto) na Mr. Godfred Mbanyi Mkurugenzi wa mafunzo (aliyeketi kulia) katika picha ya pamoja na washiriki wa semina
New Picture (92) 
Washiriki wa Semina ya utafiti wakimsikiliza mwezeshaji Dr. Eli Tumsifu toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwenye semina ya utafiti iliyofanyika katika ukumbi waTEC Kurasini Dar es Salaam tarehe. 16-20 Februari 2015
New Picture (93) 
Dr. Eli Tumsifu akiwa na washiriki wa semina ya utafiti ya PSPTB ndani ya ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe 16-20 Februari 2015
New Picture (94) 
Washiriki wa semina ya utafiti ya PSPTB wakiwa na Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB Dr. C. Tesha (aliyeketi katikati), Dr. Eli Tumsifu Mkufunzi wa semina (aliyeketi kushoto) na Mkurugenzi wa mafunzo wa PSPTB Mr. Godfred Mbanyi (aliyeketi kulia) wakati wa semina yautafiti iliyofnyika 16-20 Februari 2015 katika Ukumbi wa TEC Dar es Salaam.

Nyambui alilia riadha ifufuke upya

index 
Na Mwandishi Wetu,Morogoro MAOFISA michezo na Maofisa Elimu wa mikoa ya Tanzania wameombwa kushirikiana na wenyeviti wa mchezo wa riadha kufufua mchezo huo kutoka ngazi ya shule za msingi na Sekondari. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui akizungumza katika mkutano Mkuu wa Mwaka wa tathmini wa mashindano ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Shule za Sekondari (UMISETA) yanayosimamiwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)alisema imefika wakati kila mdau achangie kufufua mchezo huo.
Alisema mchezo huo ambao zamani ulitangaza Tanzania katika mashindano mbalimbali duniani unazidi kupoteza umaarufu kwa sababu hakuna mikakati madhubuti ya kufuatilia wanamichezo wenye vipaji kutoka ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vikuu.
Nyambui alisema kwa mara ya mwisho mwaka jana Tanzania ilishiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Scotland ikiwa ni baada ya miaka 40 kutoka na mchezaji Basil John mita 1500 kushika nafasi ya nane kati ya 12 walioingia fainali. Alisema mchezo wa riadha hauna wafadhili kama ilivyo michezo ya soka lakini amejitahidi kushawishi kampuni ya Isere Sports isaidie kuwauzia wachezaji wa riadha vifaa kwa bei ya chini.
“Tumekubaliana na Kampuni ya Isere Sports iagize na kuwauzia wetu vifaa vya michezo kwa bei ya kawaida ili wamudu kununua viatu na jezi za ” alisema Nyambui.
Meneja Masoko wa Isere Sports, Abbas Ally Isere alisema ni kweli wamefikia makubaliano hayo na yeye kama mtanzania anayehitaji vipaji vionekane atajitahidi kuhakikisha vifaa vya riadha anaviagiza na kuviuza kwa bei ya chini.
Mikoa inayotamba kutoa wanariadha wengi ni Manyara, Arusha, Mara, Mtwara, Dodoma, Mbeya, Kanda ya Ziwa na mikoa nyingine.

No comments:

Post a Comment