TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 23, 2015

Mwimbaji mchanga atamani kuimba Pasaka

imagesNa Mwandishi Wetu
MWIMBAJI chipukizi wa nyimbo za injili Victor Mbagga, amesema anatamani kupata kibali cha  kuimba kwenye miaka 15 ya Tamsha la Pasaka linalotarajia kufanyika hivi karibuni mikoa zaidi ya mitano.
Mbagga alilieleza  kuwa endapo atapata nafasi hiyo atakuwa amepata bahati ya kipekee ya kujitangaza kwa kuwa watanzania watapata nafasi ya kujua anachokifanya.
Akizungumza katika ofisi za gazeti hili Mbagga alisema kuwa ameanza kuimba tangu mwaka 2002 ambako hadi sasa ana albamu ya Usilipize Kisasi, Furaha kuwa na Yesu na Utawale Yesu ambayo itazinduliwa siku ya Pasaka. Lakini bado hajatambulika kuwa yeye ni muhubiri wa injili kwa njia ya uimbaji.
Alisema kipaji chake hakijulikani kwa sababu ya changamoto za kiuchumi hivyo anaamini kupitia Tamasha la Pasaka linaloandaliwa na magwiji wa tamasha hilo  Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar  es Salaam ataweza kujulikana kwa kuwa linakusanya Watanzania na waimbaji wengi.
Mwimbaji huyo ambaye amekusudia kufanya kazi na Msama Promotions huku akisisitiza kuwa ameona ni kimbilio kwa waimbaji wengi kwa kuwa inafanya kazi vizuri ambapo inasamabaza kazi nyingi ambazo zinafika mbali.
“Napenda kufanya kazi na mtu mwenye hofu ya Mungu jambo lingine ni kwamba  sisi waimbaji tunapata changamoto kubwa ama hatujatoka kwa hiyo wanipatie kibali cha kushiriki katika tamasha la mwaka huu waone nafanya huduma gani,” alisema Mbagga.

No comments:

Post a Comment