TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 25, 2015

Wizara yatangaza utoaji ruzuku awamu ya pili ya wachimbaji wadogo wa madini

111 
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Matokeo ya utekelezaji wa utoaji wa ruzuku kwa wachimbaji Madini wadogo nchini Awamu ya Pili yanatarajiwa kufanyiwa tathmini na ufuatiliaji kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava wakati akiongea katika Kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa kupitia Televisheni ya Taifa TBC1 mapema leo, ambapo amefafanua kuhusu taratibu za maombi ya namna ya kupata ruzuku kwa wachimbaji wadogo wa madini Awamu ya Pili. Mhandisi Mwihava ameeleza kuwa, ili kupata matokeo bora ya namna ruzuku hiyo itakavyotumiwa na wachimbaji wadogo watakaokidhi vigezo vya maombi na kunufaika na ruzuku hiyo, mpango wa BRN utatumika ipasavyo kuhakikisha kwamba fedha hizo zinatumika kama ilivyopangwa. “BRN itatumika kufuatilia utekelezaji wa ruzuku. Wizarani tuna Sehemu ya Ukaguzi wa Migodi, lakini pia tuna Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), hawa wote watashirikiana kufanya tathmini yenye matokeo tunayotarajia,” amesisitiza Mhandisi Mwihava.

Ameongeza kuwa, kiwango cha ruzuku kwa wachimbaji wadogo Awamu ya Pili kimeongezwa kufikia Dola za Marekani 100,000/-, ruzuku ambayo inalenga katika kuendeleza uchimbaji mdogo ili uwe na tija; kuwakwamua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuongeza pato la taifa. Aidha, ameeleza kuwa malengo mengine ya ruzuku hiyo kwa wachimbaji wadogo wa Madini kuwa ni kuendeleza mkakati wa kurasimisha shughuli za uchimbaji mdogo wa madini na kutoa mitaji ili kusaidia ukuaji wa tasnia ya uchimbaji mdogo wa madini. Malengo mengine ni pamoja na uongezaji thamani ya madini wenye Matokeo Makubwa Sasa. Ameongeza kuwa, Serikali imedhamiria kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini kuwawezesha kuwa wachimbaji wa kati, jambo ambalo limefanya Serikali kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika utoaji ruzuku na mikopo awamu ya kwanza. “Tunataka kuwasaidia mitaji, kuwapatia vifaa na kuhakikisha wanapata uelewa wa namna ya kufanikisha shughuli zao kupitia wataalamu wetu. Tunalenga kuwafanya wakue hadi kuwa wachimbaji wakubwa”, ameongeza Mwihava. Aidha, Mhandisi Mwihava ametumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji wadogo kuzitumia ofisi za madini zilizoko mikoani kwa ajili ya kuchukua fomu za maombi kuanzia tarehe 2 Machi na kuwataka kuzirejesha fomu hizo katika ofisi hizo ifikapo tarehe 27 Machi, 2015, zikiwa na viambatanisho vyake. Katika hatua nyingine, Mhandisi Mwihava amesema kuwa, migodi inayoshirikisha watoto wadogo katika shughuli za uchimbaji madini watanyanga’nywa leseni zao endapo itabainika kuwa, migodi hiyo inawashirikisha watoto, na hivyo kuwataka wachimbaji kufuata sheria na taratibu. “Watoto kushiriki katika shughuli za uchimbaji ni makosa. Watakaobainika watanyang’anywa leseni zao. Wizara inapinga si haki kwa watoto kufanya shughuli za uchimbaji madini”, alisisitiza Mwihava. Awamu ya pili ya utoaji ruzuku kwa wachimbaji wadogo nchini, inatekelezwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini, chini ya Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP), unaopata fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia.

No comments:

Post a Comment