TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 27, 2015

Mashindano ya gofu NIC Corporate Lugalo Challenge 2015 kufanyika kesho viwanja vya TPDF Lugalo

4Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC  Bi. Mwanaidi Shemweta akikabidhi zawadi kwa Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu  vya TPDF Lugalo tayari kwa mashindano ya NIC Corporate Lugalo Challenge 2015 yanayofanyika kesho February 28 kuanzaia saa 7:00 asubuhi kwenye viwanja hivyo yakishirikisha wachezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mpaka sasa wachezaji 60 wameshathibitisha kushiriki katika mashindano hayo na wachezaji wengine wanaendelea kujisajiri ili kushiriki katika michezo hiyo ya Gofu, Kapteni Japhet Masai ametoa mwito kwa wachezaji mbalimbali kuendelea kujisajiri na amesema wanatarajia zaidi ya wachezaji 120 watashiriki katika mashindano hayo.
 
Shindano la NIC Corporate Golf Chalennge linaandaliwa na shirika la bima la taifa NIC na  linafanyika kila mwaka kuanzia tangu lilipoanzishwa  mwaka 2013 na linashirikisha wachezaji wa rika zote na jinsia zote NIC imeandaa zawadi mbalimbali kwa washindi, ambapo mshindi wa kwanza atapata jiko kubwa la umeme. Pia wshindi wengine watapata zawadi mbalimbali zilizotayarishwa kwa ajili yao ambazo ni meza kubwa ya ofisini, mikoba  ya akina mama, mabegi ya wanafunzi, Feni , Friji, Microwave na zawadi nyingine nyingi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 5Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC  Bi. Mwanaidi Shemweta akikabidhi zawadi kwa ya jiko kubwa la umeme Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu  vya TPDF Lugalo 6Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC  Bi. Mwanaidi Shemweta na Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu  vya TPDF Lugalo wakipiga picha pamoja na zawadi hizo. 7Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC  Bi. Mwanaidi Shemweta akipiga picha mara baada ya kukabidhi zawadi hizo kwenye viwanja vya gofu  vya TPDF Lugalo.

No comments:

Post a Comment