TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, February 23, 2015

WALIMU ZAIDI YA 200 WALUNDIKANA MANISPAA YA IRINGA

index
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Bw. Ahmed Sawa akae pamoja na Afisa Elimu wake na kuwapunguza walimu 230 waliozidi mahitaji ya walimu kwenye manispaa hiyo na badala yake wawapangie kwenda vijijini.
Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Februari 22, 2015) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Ipogolo waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Ipogolo, nje kidogo ya Manispaa ya Iringa.
“Manispaa inahitaji walimu 534 lakini waliopo ni 764. Hapa kuna ziada ya walimu 230 tena kw shuke za msingi… Mkurugenzi kaa na Afisa elimu wako muwaondoe walimu waliozidi na kuwapangia waende vijijini ambako kuna mahitaji zaidi,” alisema.

“Kwa upande wa shule binafsi nako pia tatizo ni lile lile. Walimu wamezidi. Mahitaji ni walimu 75 waliopo ni walimu 142 … wanaozidi ni walimu 67,” alisema Waziri Mkuu.
“Sina tatizo na walimu wa shule binafsi kwa sababu wao wana mfumo wao wa ajira lakini hawa wa shule za Serikali ni lazima muwaondoe tena haraka sana. Waondoeni waende vijijini kwenye mahitaji makubwa sababu ualimu ni ualimu tu, siyo lazima mtu awe mjini ndiyo afundishe vizuri,” alisema.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliupongeza uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kuwa na ufaulu wa juu kwenye shule za msingi lakini akawataka wajiulize ni kwa nini ufaulu huo umeanza kushuka tangu mwaka 2013.
“Mwaka 2010 kiwango cha ufaulu kilikuwa asilimia 77; mwaka 2011 kilikuwa asilimia 87; mwaka 2012 kilipanda na kufikia asilimia 97. Lakini mwaka 2013 kilishuka hadi asilimia 82 na mwaka jana ni kama kipo palepale kwani kilikuwa asilimia 82.5. Kaeni mjiulize kumetokea nini na mtafanya nini ili kurudi tena kwenye asilimia 97 au zaidi.”
Akizungumzia suala la afya, aliwaeleza wananchi hao kwamba ameuagiza uongozi wa mkoa kupitia watoa tiba wake waweke utaratibu wa kutoa elimu walau kila baada ya miezi miwili au mitatu ili wananchi wapate ufahamu wa magonjwa makuu yanayosumbua hivi sasa.
Akifafanua magonjwa ya akinamama, Waziri Mkuu aliyataja magonjwa hayo kuwa ni saratani ya matiti, saratani ya shingo ya uzazi na tatizo la fistula wakati kwa upande wa akinababa alisema wao wanahitaji kupatiwa elimu zaidi kuhusu ugonjwa wa tezi dume.
“Matatizo haya yanatibika lakini ni lazima watu waeleweshwe kwamba wakiwahi kwenda hospitali matatizo haya yanatibika lakini wakichelewa inakuwa tatizo zaidi,” alisema.

No comments:

Post a Comment