TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 25, 2015

MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI

indexWizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika.
Halmashauri zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014. Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement – MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali
Mha. Ngosi C.X. Mwihava KAIMU KATIBU MKUU 25 Februari, 2015

No comments:

Post a Comment