
Katibu
 Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu Dkt Hamis Mwinyimvua 
akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa ya taifa(TANDTRADE)( Hawapo 
pichani) wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dar 
es Salaam.

Naibu 
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju akifatilia kikao cha 
Kamati ya Maafa ya Taifa kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam kushoto
 ni katibu wake.

Baadhi
 ya wajumbe wa Kamati ya Maafa ya taifa kutoka katika Wizara,Taasisi na 
Idara za Serikali wakifatilia kikao cha Kamati ya Maafa ya Taifa 
kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Baadhi
 ya wajumbe wa Kamati ya Maafa ya taifa kutoka katika Wizara,Taasisi na 
Idara za Serikali wakifatilia kikao cha Kamati ya Maafa ya Taifa 
kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Na Raymond 
Mushumbusi MAELEZO
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali
 imekusudia kuanzisha Wakala wa Usimamizi wa Maafa Tanzania chini ya 
Sheria ya mwaka 2004 ambao utakuwa na jukumu la kupambana na maafa 
yatakayojitokeza kwa kuratibu na kuwezesha waathirika wa maafa kupata 
misaada ya mahitaji muhimu kwa haraka.
Akizungumza
 na wajumbe wa Kamati ya Maafa ya Taifa(TANDTRADE) Katibu Mkuu Ofisi ya 
Waziri Mkuu,Sera na Uratibu Dkt Hamis Mwinyimvua amesema Serikali 
imedhamiria kuanzisha Wakala wa Usimamizi wa Maafa ili kuweka utaratibu 
mzuri ambao utasaidia kushughulikia kwa umakini maafa yatakayokuwa 
yakijitokeza katika sehemu mbalimbali nchini.
“ Ipo 
Sheria ya Wakala wa Usimamizi wa Maafa basi ni jambo jema kuwepo kwa 
Wakala ili kuweza kuratibu vizuru shughuli za kupambana na maafa 
yanayotukumba”
“Tumekutana
 leo hapa katika kikao cha kawaida cha kupata taarifa juu ya maafa 
yanayotokea nchini na tutajadili na kutoa madhimio ambayo yatatoa majibu
 ya nini kifanyike katika kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa 
kupambana na maafa” Alisema Dkt Mwinyimvua.
Kamati
 ya Maafa ya Taifa  iko chini ya mwenyekiti ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi 
ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu ikiwa na wajumbe kutoka Mamlaka ya Hali 
ya Hewa, Wizara ya Afya,Ustawi wa Jamii,Watoto na Wazee, Jeshi la Zima 
Moto,Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Wizara ya 
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na 
Michezo, Taasisi na Idara za Serikali zinazohusika na maafa.
No comments:
Post a Comment