Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,  Dk.Hamis Kigwangalla akizungumza katika mkutano wa matokeo ya ya Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,  Dk.Hamis Kigwangalla akiangalia baadhi ya vifaa tiba na dawa zilizo kamatwa katika operesheni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
 NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,  Dk.Hamis Kigwangallaameagiza
 Baraza la Wafamasia pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa 
(TFDA),kuwafikisha mahakamani wale wote waliokutwa na dawa za serikali 
katika maduka yao.
Kigwangalla
  ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kupewa matokeo ya 
Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa muhimu na yasiokuwa na vibali 
iliyofanywa na Baraza la Wafamasia na TFDA  pamoja na Jeshi la Polisi, 
amesema dawa zilizokamatwa zitaifishwe na kupeleka katika hospitali za 
serikali.
Amesema
 kuwa haiwezekani wananchi wakakosa dawa za serikali na kuonekana katika
 maduka ya dawa na watu hao wakaachwa bila kuchukuliwa hatua.
Kigwangalla
 amesema kuwa katika operesheni hiyo baadhi ya maduka yanauza dawa 
ambazo haziko kwenye orodha za dawa ikiwemo ni dawa ya usingizi ambayo 
inatakiwa kutumika wakati wa operesheni.
Aidha 
amesema kuwa baadhi ya maduka mengine yamefungwa lakini yanauza dawa 
nyakati za usiku na kuwataka wanaofanya operesheni kuendelea na 
wataokutwa wachukuliwe hatua mara moja.
Operesheni
 hiyo ilianza machi 1 hadi 3 mwaka huu ambapo walikagua maduka 685 
katika mikoa tisa na kati hayo maduka 432 yamefungiwa kwa sababu 
mbalimbali ikiwemo na kuwa na dawa za serikali pamoja na kuwa dawa za 
asili.
Aidha 
Kigwangalla amesema kuwa dawa ni sumu hivyo inatakiwa kutumika kwa 
malengo yaliyokusudiwa na wanaouza dawa ambazo hawana orodha nazo 
wanazalisha matatizo ya kiafya kwa wananchi.
Kigwangalla
 amesema hadi sasa ni dawa 65 tu ndiyo zenye nembo ya serikali na 
kuwataka wananchi kutoa ushirikiano pale watakapopata dawa serikali 
katika duka la dawa.
Amesema
 kuwa jeshi la polisi lichukue hatua ya kuwabana wale wote  waliokutwa 
na dawa za serikali kuwabana katika kuweza kuwapata waliokuwa wakiwapa 
dawa hizo.
No comments:
Post a Comment