Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Joyce Thobias na mwanae Jonathan 
Mbarak ambaye amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Chato akimuuguza 
mwanae majeraha ya moto Machi 16,2916. mheshimiwa Majaliwa alikuwa 
katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Geita.
Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha gari la wagonjwa likiwa ni moja kati ya 
mawili yaliyotolewa msaada na Bibi Merete Trolle wa Denmark akisaidiwa 
kulisafilisha hadi hapa nchini na Mgodi wa Geita Gold Mine. Makabidhiano
 hayo yalifanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi 16, 2016.
Waziri
 Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua duka la dawa la MSD baada ya kulizindua 
kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi 16, 2016. Kulia ni Mwenyekiti 
wa Bodi ya MSD, Profesa Mtulia.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliiwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Chato , Machi 16, 2016.
No comments:
Post a Comment