
Waziri
 wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na 
wauzaji wa filamu za nje kuhusu kufuata sheria ya uuzaji wa filamu hizo 
hapa nchini katika kikao kilichofanyika  leo jijini Dar es 
Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo.

Katibu
 Mtendaji Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo akieleza jambo wakati kikao 
kati ya Serikali na wauzaji wa Filamu za nje(Hawapo Pichani) 
kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam .Kulia kwake ni Mkurugenzi wa 
Bodi hiyo Bw Tairo.

Mwenyekiti
 wa  wauzaji wa filamu za nje Bw Joseph  Lyakurwa akiwasilishwa mada kwa
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe.Nape Nnauye wakati wa
 kikao baina ya Serikali na wauzaji wa filamu hizo  kilichofanyika leo 
jijini Dar es Salaam.

Baadhi
 ya wauzaji wa Filamu za nje  walioshiriki katika kikao kati yao na 
Serikali cha kubadilisha sheria ya uuzaji wa filamu za nje hapa nchini 
kilichofanyika leo jijjini Dar es Salaam.
Na: Shamimu Nyaki
Kufuatia
 kuwepo kwa Filamu nyingi za nje zinazouzwa hapa nchini  bila kufuata 
Sheria ya uuzaji wa kazi hizo Serikali imewataka wauzaji hao kufanya 
biashara hiyo kwa kufuata na kuzingatia sheria iliyowekwa ili kusaidia 
kukuza na kutangaza filamu za hapa nchini.
Hayo 
yamesemwa leo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape 
Nnauye wakati alipokuwa akizungumza na wauzaji wa Filamu hizo leo jijini
 Dar es Salaam.
Amewataka
 wauzaji hao kuwa na  mkataba pamoja  wamiiki wa kazi hizo ili waweze 
kufanya biashara hiyo kwa uhalali kwakua Serikali itawasaidia kusimamia 
utekelezaji wa mikataba hiyo na kurahisisha utekelezaji wa sheria 
iliyopo.
“Lazima
 mfuate na kutekeleza Sheria iliyopo kwakua mimi nipo hapa kuisimamia na
 kuhakikisha sheria hiyo inatekelezwa”.Alisema Mhe.Waziri Nape.
Aidha 
katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi Joyce Fissoo ameongeza kuwa ni 
lazima wauzaji wa filamu hizo kuhakikisha kuwa filamu wanazouza 
zimehakikiwa na bodi ya filamu pamoja na COSOTA ili kudhihirisha ubora 
wa kazi hizo na viwango vya hapa nchini.
“Ni 
lazima muhakikishe kazi mnazouza zimeruhusiwa na Bodi ya filamu pamoja 
na COSOTA  na zinafuata  madili ya hapa nchini’’.Aliongeza Bi. Joyce.
Ameongeza
 kuwa bodi ya Filamu pamoja na COSOTA  wapo tayari kuwasaidia kupata 
haki miliki ya filamu hizo wanazouza kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya 
kuruhusu filamu gani inastahili kuuzwa na ipi haistahili kuwepo sokoni.
Uuzaji
 wa filamu za nje hapa nchini umechangia kwa kiasi kikubwa filamu za 
hapa nchini kukosa soko hali inayochangia kudidimia kwa sanaa hiyo hapa 
nchini ambayo inatoa ajira nyingi kwa vijana.
No comments:
Post a Comment