Teknolojia inazidi kukua na watu hawajaridhika kabisa na kile kinachoonekana duniani kuwa ni mageuzi.
Mjasiriamali wa Marekani ambaye ni mzaliwa wa Afrika Kusini,
billionaire Elon Musk ambaye amegundua teknolojia ya mwendo kazi wa hali
ya juu ‘The Hyper loop’ amekuja na wazo la kuunda treni ambayo itakuwa
na mwendo mara mbili ya mwendo kasi wa ndege za kawaida.
Mara tu treni hiyo itakapotengenezwa kwa teknolojia hiyo ya mwendo
kasi, itakuwa na uwezo wakuondoka mara tu abiria watapokuwa ndani ya
treni hiyo kwa idadi inayotakiwa bila kusubiri ratiba baalum kama ilivyo
kwa treni za umeme nchini Marekani.
Elon Musk ameeleza kuwa endapo teknolojia hiyo itakubalika na kupitishwa
chombo hicyho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria kutoka Los Angeles
hadi San Francisco ndani ya nusu saa tu!! Mwendo ambao kwa kawaida ndege
hutumia zaidi ya saa moja. inaweza kutoka New York hadi China kwa muda
wa saa mbili tu.
Kwa maelezo ya Elon Musk, wengi wanamuona kama amechanganyikiwa na pesa
hivi lakini baadhi ya engineers wanaonekana kuiamini idea yake kwa kiasi
fulani hasa baada ya kuona vifaa alivyonavyo na kuelekeza jinsi
itakavyofanya kazi.
No comments:
Post a Comment