Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au namba +255767869133.
SERIKALI
ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imeiomba Serikali ya Ujerumani kupanua
uwekezaji katika nyanja za viwanda vidogo vidogo pamoja na bahari kuu
ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad
alitoa ombi hilo alipokutana kwa mazungumzao na Balozi wa Ujerumani
nchini, Egon Kochanke aliyefika kwa ajili ya kujitambulisha.
Maalim Seif alisema miongoni mwa matatizo makubwa yanyoikabili
Zanzibar kama nchi nyingine za Afrika ni vijana wengi kukosa ajira na
shughuli za kujiletea maendeleo, hivyo Ujerumani inayo nafasi kubwa ya
kupambana na jambo hilo.
Hata hivyo, alisema miongoni mwa njia muafaka ya kuweza kufanikisha
azma hiyo, ni nchi hiyo kuelekeza nguvu zaidi katika kusaidia elimu ya
amali ambayo itawawezesha vijana wa Zanzibar wakiwemo wale wanomaliza
masomo kuweza kupata mbinu za ajira.
Aliongeza kuwa Zanzibar imeweza kupiga hatua kubwa katika sekta ya
elimu lakini bado inayotolewa haijakuwa na ubora unaowezesha vijana
kukabiliana na changamoto za uhaba wa ajira.
Seif alisema fursa nyingine muhimu za ushirikiano kati ya nchi mbili hizo ni katika sekta ya utalii na kilimo.
Naye Balozi Konchanke alisema amepokea maombi hayo na yatazingatiwa katika mipango ya ushirikiano wa nchi yake na Tanzania.
Alisema anaelewa kuwa Zanzibar inazo fursa muhimu za kiuchumi na
biashara, ikiwemo kilimo cha viungo na utalii ambazo wawekezaji wa
Ujerumani wanaweza kuzitumia katika kufungua miradi yao.
Alisema kuwa atakuwa balozi katika kuiuza Tanzania na Zanzibar kwa
wawekezaji wa Ujerumani kwani wanaweza kuzitumia kwa kufungua miradi
yao.
Chanzo:Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment