Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au namba +255767869133.
JESHI la Magereza mkoni Dodoma, limewataka wakulima na wafugaji wa
mkoa huo kufika katika maeneo yao ya bustani ya ufugaji ili kupata elimu
ya kisasa ya ukulima na ufungaji bora.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Magereza mkoa wa Dodoma, Kibwana
Kamtande, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu
ya kilimo na ufugaji bora kwa wakulima na wafugaji mkoani hapa.
Kamtande alisema licha ya jeshi hilo kutoa huduma kwa wafungwa pekee
lakini pia limejikita kutoa huduma ya elimu ya kilimo na ufugaji kwa
wananchi wa mkoa huu.
Kwa mujibu mkuu huyo, magereza zote za wilaya za mkoa wa Dodoma
zimekuwa kikijishughulisha na kilimo na ufugaji sambamba na shughuli za
kiujasiriamali kama utengeneza wa viatu, kufuma vitambaa na mashuka,
utengenezaji wa majiko na sabuni na ufyatuaji wa matofali.
“Wananchi wasiwe na fikra potufu juu ya jeshi hili bali waungane na sisi katika suala zima la kujikwamua na umasikini,”alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment