Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akizungumza katika
Kongamano hilo kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Picha na OMR
Waziri
wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, akizungumza katika
Kongamano hilo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufungua kongamano hilo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake ya ufunguzi wakati akifungua Kongamano la siku tatu
la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala mbalimbali
yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, ambapo Tanzania
imeteuliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo la tatu la Kimataifa la
Mtandao wa Wanasayansi Vijana Duniani (YES). Aidha Kongamano hilo
lililoshirikisha jumla ya wajumbe zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya
nchi pia, litajadili usimamizi wa Rasilimali mbalimbali zikiwemo Mafuta
na Gesi. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya sanamu la mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa
Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi
Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana,
linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini,
linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo. Picha na OMR
Rais
Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa, akipokea zawadi ya
picha ya mnyama kutoka kwa Rais wa wa Mtandao wa Wanasayansi Vijana
Duniani (YES), Meng Wang, wakati wa ufunguzi rasmi wa Kongamano hilo, la
siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana, linalojadili masuala
mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini, linaloendelea kwenye Ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal (kushoto) ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi ya ramani ya Afrika, Rais wa wa Mtandao wa
Wanasayansi Vijana Duniani (YES), Meng Wang, baada ya kufungua rasmi
Kongamano hilo, la siku tatu la Kimataifa la Wanasayansi Vijana,
linalojadili masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini,
linaloendelea kwenye Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment