Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au namba +255767869133.
Mwenyekiti wa Jamii ya Wafugaji, Huruma Ole
Kalaita, akielezea maoni ya wafugaji wanayotaka yaingizwe kwenye Katiba
Mpya mjini Dodoma jana.
Wafugaji kutoka maeneo mbalimbali nchini
wamewasilisha mapendekezo na maoni yao kwa Bunge Maalumu la Katiba
wakitaka yaingizwe kwenye rasimu ya katiba.
Wafugaji hao, ambao walifika ofisini kwa viongozi wa Bunge hilo mjini Dodoma jana, waliwataka wajumbe wa Bunge hilo kuwa na hofu na Mungu pindi wanapojadili sura mbalimbali za rasimu ya katiba.
Akiwasilisha mapendekezo hayo, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji nchini, Kasundu Wamalwa, alitaka katiba mpya itambue mila na tamaduni za wafugaji wa asili.
Alisema wanategemea katiba itakayotambua wafugaji wa asili wa Tanzania.
“Maridhiano na utashi wa kisiasa ndiyo utakaoleta katiba bora ya Watanzania… na katiba bora ndiyo kimbilio la wafugaji na Watanzania kwa ujumla,” alisema.
Naye mmoja wa wafugaji hao, Samson Seba, alisema licha ya wafugaji kulisha taifa hili, wamekuwa wakiuawa na kunyanyaswa na makundi mbalimbali, wakiwamo wawekezaji.
Alisema madaktari, walimu na makundi mengine huwa yakigoma hayaguswi, lakini wafugaji wamekuwa ni watu wa kushikiwa mitutu ya bunduki na mabomu.
Mwenyekiti wa Wafugaji hao, Huruma Ole Kalaita, alisema hawatakuwa tayari kuipokea rasimu ya katiba kama haitajumuisha haki za wafugaji.
Akijibu hoja za wafugaji hao, mmoja wa viongozi wa Bunge hilo, alisema Rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba ilishatambua haki za wafugaji kwenye Sura ya Pili ibara ya 10.
Hata hivyo walisema, mawazo yaliyotolewa na wafugaji hao yatajumuishwa kwenye katiba hiyo.
Mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda (pichani), ambaye ndiye aliwapeleka wafugaji hao bungeni, alisema ataendelea kuwatetea wakulima na wafugaji, ambao wana matatizo ya msingi.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment