Waziri
wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (wakatikati)
katika ziara ya kutembele mabaa na mahoteli ya kitalii, kutokana na
wananchi kulalamikia vitendo vya upigwaji wa ngoma na vitendo viovu,
(kulia) Mkuu wa Wilaya Kaskani (B) Unguja Khamis Jabir Makame na kushoto
ni Sheha wa Kiwengwa Bw. Maulid Masudi Ame huko Kiwengwa.
Waziri
wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk na Mkuu wa
Wilaya ya Kaskazini B, Khamis Jabir Makame wakipapa maelezo kutoka kwa
mmiliki wa Baa ya Vision Pub Francis Vicoguga juu ya undeshaji wa kazi
zake katika Baa hiyo.
Waziri
wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk,akizungumza na
wananchi na wamiliki wa mahoteli na baa katika kijiji cha Kiwengwa mara
baada ya ziara yake ya kutembelea hoteli hizo.
Mratibu
wa Wanawake na Watoto Bi Mtumwa Rashid Khalifa ,mkaazi wa Kiwengwa
akizungumzia kero wanazozipata kutokana upigwaji wa madisko katika mabaa
kijijini hapo.(Picha na Jamila Abdalla – Maelezo Zanzibar).
Na Ali Issa Maelezo-Zanzibar. 15/8/2014.
Waziri
wa Habari,Utamaduni , Utalii na Michezo Saidi Ali Mbaruok amepiga
marufuku shughuli zote za upigaji wa disko katika eneo la kiwengwa mpaka
pale Serikali ya wilaya itapo toa maelekezo maalumu ya upigaji wa disko
hilo kwa utaratibu unao faa.
Agizo
hilo amelitoa leo huko kiwengwa Mkoa wa kaskazini “A”wilaya ya
kaskazini B Unguja katika Ofisi ya umoja wa maendeleo wa kijiji cha
kiwengwa wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa mabaa
mikahawa,na kumbi na starehe juu ya kukithiri wa upigaji wa magoma
kucha.
Amesema
amelazimika kuzifunga shughuli zote za upigaji wa madisko usiku
kutokana na kutokua na utaratibu mzuri wa upigaji ngoma hizo usiku
haliambayo
inapelekea wageni wa kitalii na wenyeji kuchukia hali hiyo kwa kukosa
usingizi na kusumbuliwa wagonjwa wenye shindikizo la damu.
Amsema
hali hiyo haiwezekani kuona inaendelea katika hali kama hiyo kwani
inapoteza muelekeo na mstakabali mwema wanchi na raia kwaujumla.
“Nimepokea
messsege ya kwamba watalii wamefika kusema wanaondoka na kutafutiwa
sehemu nyengine wakapunzike kutokana na zogo kuwa jingi la madisko,hili
hiliwezekani liendelee”lisema Waziri.
Aidha
alisema haiwezekani kuona utamaduni wa burudani unavurugwa kituambacho
ni kosa kufanya hivyo na kwenda kinyume na taratibuzao selka zao.
“kuazia
leo napiga marufuku mpaka sheha wa shehia hii aridhie hata kama kuna
kibali ,kwani sheha yeye ndio anae jua hali za raia wake kuna wagonja,na
wenyemaradhi ya kuhitaji kupumzika hatutaki kuona masuala yasio na
utaratibu.”aliongeza Waziri.
“mimi
kazi yangu ni kuutangaza utalii nasio utalii uharibiwe ,tufahamu kua
ulalii Zanzibar ndio uchumi unao tegemewa kwa sasa kwa hivyo
tulinde,”aliongeza Waziri Said.
Hata
hivyo waziri huyo alichukia vitendo vya uwasharati vilivyo tapakaa
katika kijiji hicho na kujenga mabaa karibu na nyumba za ibada kitu
ambacho aliagiza kwa mkuu wa wilaya kuyafanyia kazi.
Nao
wazazi wa kiwengwa Othumani mnyanja na mtumwa Rashidi walisema kiwengwa
hivisasa imepoteza muelekeo kwani watoto wao wanaishia katika madisko
na kukosa masoma kitiambacho ni hatari kwao.
Aidha
walisema kua watoto wao wakiwa na umri mdogo na kujishughulisha na
masuala ya kimapezi jambo linalo wafanya nialama ya kupotea na kuacha
mila za kislamu.
Wakitaja maeneo ya nayopigwa miziki na watoto wao kwenda ni pamoja na maeneo
yanayo pigwa madisko hayo ni pamoja na ,kigorofani, vishani wazalendo
pub, Kamili View,Obama Baa na kigorofani eneo la mafarasi.
Nae miliki wa ukumbi wa Disko wa PERUU B, Peruce Osward Buhoma akiulizwa
swali na waziri kwanini anafanya mazogo usiku alikiri kwa kusema
hufanya hivyo kwaajili ya kuvuta wateja na kufanya ushindani kila mmoja
kwajili ya kusikika zaidi kuliko mweziwe.
Bibbi
huyo na wezake walisema wanaweza kujirekebisha lakini pawe na utaratibu
wa kupiga madisko kwa zamu na utaratubu mzuri utakao wekwa na uongozi.
No comments:
Post a Comment