Mshambuliaji wa timu ya Kombaini ya Tanga, Kassim Jumaa
(kushoto), akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Survey veterani, Ahmad Rasuli
(katikati), wakati wa mchezo maalum wa kusherehekea Sikukuu ya Wakulima Nanenane
uliofanyika kwenye viwanja vya Disuza mjini Tanga. Mchezo huo ulidhaminiwa na
NSSF. Kuilia ni Amir Athuman wa Kombaini ya Tanga.
Na Elizabeth Kilindi, Tanga
Na Elizabeth Kilindi, Tanga
Timu ya Survey Veterani ya jijini Dar es salamu imeifunga timu ya Kombaini vijana Veterani ya Jiji la Tanga 2-1 katika mchezo wa kuazimisha sherehe za wakulima nane nane viwanja vya Disuza vilivyopo Mkoani Tanga.
Mchezo huo ambao umedhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ulikuwa na lengo la kukutanisha timu za maveterani ili kujenga mshikamano na kuhamasisha michezo.
Katika mchezo huo wachezaji wa savey Carlos Mdinga alijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na wapinzani hatua ambayo ilisababisha gori hilo Dakika ya pili.
Aidha katika mchezo huo timu ya Savey ilionyesha makali yake ambapo dakika ya 40 walisawazisha goli kutoka kwa kiungo wake Silyvester Malango.
Hata hivyo bahati nyota ilizidi kungaa kwa timu ya veterani baada ya Dakika ya 70 kupata goli la pili lililotiwa nyavuni namshambuliaji wake David Emanuel.
Katika mchezo mwengine ni kati ya Timu ya Best point veterani imeibuka na ushindi wa goli mbili dhidi ya Kombaini ya wazee Veterani ya Jijini Tanga.
Magoli ya Best point yalifungwa na Sadiki Salumu dakika ya saba na goli la pili lilifungwa na Miraji Paulo dakika za lala salama.
Baada yakumalizika kwa mchezo huo kocha Seleman Mgaya ambaye ni Katibu wa Survey Veterani ya Dar es salaam amesema wamefurahishwa ushirikiano unaotolewa namfuko wa hifadhi ya jamii NSSF hasa kwa kuonyesha mchango wao katika michezo.
“Tunaishukuru sana NSSF kwa moyo wa kutukutanisha pamoja kimichezo hatua ambayo tunajivunia kwaniwao wametambua umuhimu wetu hivyo hatuna budi kutoa ushirikiano”amesema Mgaya.
No comments:
Post a Comment