Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au namba +255767869133.
WAKULIMA
mkoani Ruvuma wameshauriwa kujiunga kwenye vikundi ili waweze kukopa
zana za kisasa za kilimo yakiwemo matrekta aina Power Teller, mashine za
kisasa za kupukuchua mahindi ili kuweza kuongeza tija uzalishaji kwani
kilimo ni biashara hivyo kuweza kujiongezea kipato.
Ushauri huo ulitolewa
na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bapt Company Mkoa wa Ruvuma, Ayoub Mbilinyi
ambayo inajishughulisha na uuzaji na usambazaji wa zana za kisasa za
kilimo alisema ili wakulima waweze kuzalisha mazao kwa wingi wanapaswa
kubadilisha kilimo chao na kulima kilimo cha biashara kwa kutumia zana
za kisasa za kilimo.
Mbilinyi aliongeza kuwa
kampuni hiyo inatoa mkopo kwa vikundi na mwananchi mmoja moja ambapo
wanachoangalia ni vyanzo vyake vya mapato lakini kwa mkulima anaweza
akatoa asilimia 70 ya malipo ya awali ambapo kiasi kinachobakia atalipa
kulingana na makubaliano maalumu watakayokubaliana au baada ya mavuno
ambapo zana hizo zinapatikana wakati wote ambapo mteja akitoa oda yake
anapatiwa zana hizo ndani ya siku saba.
Alisema wakulima hao
wanaweza kujiunga na kukopa matrekta makubwa 45hp-95hp(4WD) kwani ni
imara na zina nguvu na zinatumia mafuta kidogo badala ya kung'ang'ania
kutumia jembe la mkono kwani limeshapitwa na wakati.
"Bado mkoani Ruvuma
wakulima hawana mwamko wa kutumia zana za kisasa za kilimo nawashauri
wakulima wabadilike na kuanza kutumia zana za kisasa za kilimo kwani
mbali na kuuza pia tunakopesha vifaa mbali mbali vya kilimo matrekta,
powertiller aina ya Maize Thresher kwa bei nafuu kwani mkulima anaweza
kununua kwa kiasi cha sh. milioni 5.5, mashine za kisasa za kupukuchulia
mahindi, mashine za kupanda mpunga; na kuvunia mpunga, mashine za
kuvuna ngano pamoja na pampu za kumwagilia maji ambapo matarajio yao ni
kuhakikisha wanasambaza pembejeo za kilimo zikiwemo dawa,mbolea pamoja
na mbegu," alisema.
Aidha, aliwashauri
wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kununua vipuri vya matrekta mbali mbali
ambavyo havipatikani mkoani humo kwenye kampuni hiyo.
Chanzo:Majira
No comments:
Post a Comment