Yussuf Manji kulia na makamu wake, Clement Sanga |
1.
Mwenyekiti na Makamo Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Sports Club
(YANGA) kwa mamlaka waliyopewa na Wanachama,kubadilisha, kupunguza au
kuongeza Mjumbe yeyote kwenye Kamati ya Utendaji wakati wowote,kulingana
na changamoto wanazoziona zinazoikabili Klabu ya YANGA, Mwenyekiti na
Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kutoa taarifa rasmi, kuwa Kamati ya
Utendaji ya YANGA na Kamati zote ambazo ziko chini ya Kamati ya
Utendaji zitavunjwa kuanzia tarehe 31 Julai, 2014.
2. NVile vile, Mwenyekiti na
Makamo Mwenyekiti wa YANGA wanapenda kuwashukuru Wajumbe wote wa Kamati
ya Utendaji ya YANGA kwa juhudi zao za kutekeleza shughuli za Klabu.
3. Wakati huo huo, Mwenyekiti
wa Klabu ya YANGA Bw.Yusuf Manji na naibu wake Bw.Clement Sanga
wanatangaza Kamati ya Utendaji mpya ya Young Africans Sports Club ambayo
itakuwa madarakani kuanzia 1 Agosti, 2014 kama inavyoelezwa na kila
Mjumbe anavyotajwa hapo chini anakuwa na majukumu ya msingi ya kusimamia
kama inavyoonyeshwa pembeni ya jina lake.
WAJUMBE WAPYA WA KAMATI YA UTENDAJI YA YANGA NI HAWA WAFUATAO:
1.Bw.Abubakar Rajabu - Mradi wa Jangwani City
2.Bw.Sam Mapande - Sheria na Utawala Bora
3.Bw.George Fumbuka - Uundwaji wa Shirika
4.Bw.Waziri Barnabas - Vibali vya Hatimiliki na Mahusiano na Wafadhili
5.Bw.Abbas Tarimba - Mipango na Uratibu
6.Bw.Isaac Chanji na Bw.Seif Ahmed - Uendelezaji wa Mchezo
7.Bw.Musa Katabalo - Mauzo ya Bidhaa
8.Bw.Mohammed Bhinda - Ustawishaji wa Matawi
9.Bw.David Ndeketela Sekione - Uongezaji wa Wanachama
10.Bw.Mohammed Nyenge - Utangazaji wa Habari, Taarifa, Matangazo n.k.
WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI ILIYOUNDWA UPYA WATASIMAMIA KIMSINGI KAMATI NDOGO ZIFUATAZO:
•Kamati ya Maadili - Bw.Sam Mapande
•Kamati ya Nidhamu - Bw.Sam Mapande
•Kamati ya Uchaguzi - Bw. Sam Mapande
•Kamati ya Uchumi na Fedha - Bw.George Fumbuka na Bw.Waziri Barnabas
•Kamati ya Mashindano - Bw.Seif Ahmed & Bw.Isaac Chanji
•Kamati ya Soka la Vijana na Wanawake - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
•Kamati ya Ufundi - Bw.Seif Ahmed &Bw.Isaac Chanji
5. Mwenyekiti na Makamo
Mwenyekiti wa YANGA wanamategemeo makubwa kuwa waliotajwa hapo juu
watahakikisha wana timiza malengo yaliyokusudiwa na YANGA ili“DAIMA
MBELE, NYUMA MWIKO” mpaka hapo itakapoamuliwa kubadilishwa au
kutenguliwa vinginevyo.
6. Mwisho,tunawaomba
ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha kuwa YANGA inapiga hatua mbele na
inafanikiwa katika kufikia malengo na mipango yake ya maendeleo ya muda
mfupi na ya muda mrefu kwa manufaa ya Klabu, Timu na wana YANGA popote
walipo duniani.
“MUNGU AIBARIKI YANGA.”
(BENO NJOVU)
KATIBU MKUU- YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
No comments:
Post a Comment