Mashindano ya Mijadala kwa kwa vyuo vya Elimu ya Kati kwa kanda ya Dar es Salaam, yanatarajiwa kuanza Novenber mwaka
huu.
Akizungumzia
katika semina elekezi, iliyowakutanisha baadhi ya walimu wa mijadala
kutoka katika Vyuo mbalimbali, Mratibu
wa Tamasha la Nacte Inter College Tanzania 2014/2015, Magreth Kilawe,
kutoka Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania, ambao ndio waandaji wa
Tamasha hilo, Bi Magreth Milawe, amesema jumla ya Vyuo 33 kutoka Kanda
ya Dar es Salaam,Vimeshathibitisha ushiriki wao katika Tamasha hilo
ambalo ni la kwanza kufanyika Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Mratibu wa Tamasha la NACTE INTER COLLEGE TANZANIA 2014/2015: Bi, Magreth Kilawe |
Bi, Magreth,
amesema Tamasha hilo pia litaonyeshwa kwenye moja ya runinga hapa
nchini kuwapa fursa watazamaji kushuhudia vipaji vya wanafunzi katika
kujieleza mbele ya jamii.
Amesema
nia na madhumuni ya Tamasha hilo, mbali na kuondoka na kitita cha
zawadi kwa washindi lakini pia ni njia mojawapo ya kuinua kiwango cha
elimu hapa nchini kwa wanafunzi kupata nafasi ya kujieleza mbele za
watu, kufanya utafiti kutokana na mada itakayowekwa mezani, kuweka
mahusiano mema dhidi ya wanafunzi na kujenga kizazi kipya katika nyanja
ya elimu kupitia mfumo wa mijadala.
Bi, Magreth Kilawe(kulia) kushoto ni Mwakilishi wa Viongozi Serikali ya Wanafunzi Mr.Stephano |
Vyuo vilivyojitokeza mpaka sasa miongoni mwa vyuo 105 kushiriki Tamasha hilo mpaka sasa ni
22. Bagamoyo College of Arts - Bagamoyo (Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
(TaSUBa) - Bagamoyo) National College of Tourism, Bustani - Dar es Salaam
26.Lugalo
Military Medical School - Dar es Salaam
32. Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) - DSM
Kwa
Mujibu wa Bi, Magreth,nafasi za ushiriki bado zipo kwa vyuo ambavyo
bado havijathibitisha ushiriki na kwamba mwisho wa Usajili ni tarehe
moja mwezi wa tisa mwaka huu.
Maandalizi yanaendelea vizuri mpaka sasa tunaendelea na mazungumzo na wadhamini na ambao tayari wameonyesha nia ya kusaidia Michezo hii ya NACTE katika vyuo vya Elimu ya Kati ni Pamoja na N.M.B, P.S.P.F, TCRA,AZAM, CXC TOURS,PCCB,LAPF,TAHA, BANK YA POSTA,MALT MEDIA GROUP, NSSF,TTCL,FAST-JET,IKONDOLELO LODGE, Global Publishers, East Afrika Radio Radio & TV,Clouds Media Group"pamoja na mtandao wa www.shaabanmpalule.blogspot.com(FULL UTAMU-JUMWAGE), ameongeza Bi, Magreth
Maandalizi yanaendelea vizuri mpaka sasa tunaendelea na mazungumzo na wadhamini na ambao tayari wameonyesha nia ya kusaidia Michezo hii ya NACTE katika vyuo vya Elimu ya Kati ni Pamoja na N.M.B, P.S.P.F, TCRA,AZAM, CXC TOURS,PCCB,LAPF,TAHA, BANK YA POSTA,MALT MEDIA GROUP, NSSF,TTCL,FAST-JET,IKONDOLELO LODGE, Global Publishers, East Afrika Radio Radio & TV,Clouds Media Group"pamoja na mtandao wa www.shaabanmpalule.blogspot.com(FULL UTAMU-JUMWAGE), ameongeza Bi, Magreth
Michezo
mingine katika tamasha hilo ni pamoja na Soka,
Netball,Basketball,Handball, Voleyball, Marathoni,Vipaji vya
Utangazaji,Mashindano ya DJ's, Shindano la Mavazi ya Ofisini,Uongozi na
Utawala, pamoja na Vipaji vya Kuimba (Muziki).
Fulsa
hiyo ya uwepo wa michezo kwenye vyuo vya elimu ya kati Tanzania,
imekuja baada ya hitaji la muda mrefu kutoka kwa wanafunzi waliokuwa
wakitoka kwenye Shule za Sekondari kujiunga katika Vyuo vya Elimu ya
Kati, ambapo walikuwa hawapati fulsa ya kukutana kimichezo katika
kubadilishana mawazo na kutengeneza mahusiano mema miongoni mwa
Wanafunzi, Walimu na Wadhamini.
Hata
hivyo Bi, Magreth amesisitiza kwamba, wakati wa Tamasha Msisimko mkubwa
utakuwa kwa washiriki wa Mijadala(Debate Competition)na kwamba baada ya
kukamilika tamasha la Kanda ya Dar es Salaam, itafuata Kanda ya Mikoa
ya Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma na Zanzibar,katika kipindi cha 2014/
2015.
Michezo yote itachezwa kwenye viwanja vilivyopendekezwana Kamati Kuu ya NACTE INTER COLLEGE TANZANIA, mbavyo ni
The Mwalimu Nyerere Memorial
Academy, University of Dar es Salaam, TCC Chang’ombe, Kibaha Secondary,
Gymkhana Posta, na Leaders Club.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu mchimati@gmail.com au namba +255767869133.
No comments:
Post a Comment