TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 5, 2014

Airtel yazindua huduma ya Breaking news kupitia simu

IMG_0731Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Mwananchi, Francis Nanai akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakati wa uzinduzi wa huduma ya kuwapasha habari wananchi kwa njia ya simu (Breaking News) iliyofanyika katika ofisi za Mwananchi jijini Dar es Salaam
……………………………………………………………
Airtel yazindua huduma ya Breaking news kupitia simu Dar es Salaam, Airtel imezindua huduma mpya ya utaoaji wa taarifa za hapo kwa papo . Huduma hiyo inayojulikana kama Airtel Mwananchi Breaking news itahusisha utoaji wa habari kupitia wateja wa simu za mkononi wanaotumia mtandao wa Airtel kwa kushirikiana na Kampuni ya Mwananchi Communications inayochapisha magazeti ya Mwananchi.
 Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mwananchi Francis Nanai alisema pamoja na mambo mengine mpango huo unalenga kuwafikisha watanzania habari sahihi kwa wakati.
Alisema kwa kutambua maendeleo ya teknolojia matumizi ya simu za mkononi katika kutoa taarifa yanazidi kuongezeka na kuwa sehemu ya maisha ya kila siku. <  Kadiri siku zinavyokwenda teknolojia inaonekana kukua na simu za mkononi kutumika kama njia mojawapo ya kuwasilisha taarifa kutokana na hilo Mwananchi kwa kushirikiana  na Airtel tumekuja na ushirikiano huu ambao utawawezesha wateja wetu kupata taarifa sahihi na kwa wakati > alisema Nanai Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso  alisema kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kubuni njia mbalimbali zinazorahisisha utoaji wa huduma za mawasiliano na taarifa kwa wateja wake. Alisema kupitia huduma hiyo watanzania watapata fursa ya kupata habari zinazotokea hapo kwa papo kutoka katika kila kona ya dunia. Airtel tuko mstari wa mbele kuanzisha huduma ambazo zinalenga kumrahisishia mawasiliano mteja  na kupitia huduma hii ni matumaini yangu watanzania watapata nafasi ya kupata habari mahali popote walipo >alisema Colaso Alisema kwa kuanzia wateja wa Airtel watapata huduma hiyo bure kwa muda wa siku saba na baada ya hapo watatozwa Sh 120 kwa siku.
 Meneja Masoko wa MCL Bernad Mukasa alisema taarifa zitakazotolewa kwa wateja wa Airtel zitakuwa katika sehemu tatu hivyo mteja atakuwa na uamuzi wa kuchagua habari anazozitaka ambazo zitahusisha habari za kawaida,burudani na michezo.
<  Sasa hivi wateja watakuwa na uamuzi wa kuchagua taarifa wanazohitaji kama ni habari za kawaida,michezo au burudani kwa mujibu wa matakwa ya kila mmoja >alisema Mukasa

No comments:

Post a Comment