TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 3, 2014

MWIGULU NCHEMBA NA MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA KALENGA WASHIRIKI MAZISHI YA VIJANA WATATU KATIKA KIJIJI CHA KIDAMALI MKOANI IRINGA

5Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga Bw. Godfrey Mgimwa akisalimiana na waombolezaji mara baada ya kuwasili katika kata ya Nzihi Kidamali ambako walienda kushiriki katika mazishi ya vijana watatu wa kijiji hicho waliofariki kwa ajali jana mkoani Iringa, marehemu hao ni Nyakile Luvanda Dereva, Sabasaba Kunzula Kuli, Ansikali Chengula Kuli waliokuwa wakifanya kazi katika kiwanda cha Maji Afrika yanayotengenezwa Kidamali mkoani humo, Katika Mazishi hayo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchema ametoa shilingi milioni moja kama rambirambi kutoka Chama cha Mapinduzi huku akimshauri mgombea ubunge wa jimbo la Kalenga  kupitia CCM ndugu Godfrey Mgimwa kuchukua jukumu la kulipia karo za watoto wa familia za marehemu endapo atashinda kiti hicho na kuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga. 6Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey Mgimwa wakiwasili katika kijiji cha Kidamali wakati walipoenda kushiriki mazishi ya wananchi watatu wa kijiji hicho waliofariki kwa ajali jana. 9Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba akizungumza na wanachama wa Chama cha CHADEMA mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kidamali. 10Majeneza ya miili ya vijana waliofariki kwa ajali katika kijiji cha Kidamali mkoani Iringa yakiwasili katika eneo la makaburi mahali ambapo mazishi yamefanyika. 11Majeneza ya miili ya vijana waliofariki kwa ajali katika kijiji cha Kidamali mkoani Iringa yakiwasili katika eneo la makaburi mahali ambapo mazishi yamefanyika. 12Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati waliowasili katika makaburi 13Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati waliowasili katika makaburi 14Majeneza ya miili ya vijana waliofariki kwa ajali katika kijiji cha Kidamali mkoani Iringa yakiwasili katika eneo la makaburi mahali ambapo mazishi yamefanyika. 15Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba akishiriki mazishi hayo 
 16 
Watoto wa mmoja wa marehemu wakiaga mwili wa baba yao huku wakilia kwa uchungu. 
 17 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba na mgombea ubunge wa jimbo hilo Godfrey Mgimwa wakishiriki mazishi hayo. 18Umati wa waombolezaji ukiwa makaburiki ukishiriki katika mazishi hayo. 19Umati wa waombolezaji ukiwa makaburiki ukishiriki katika mazishi hayo. 20Mazishi ya miili hiyo yakiendelea. 21Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba na mgombea ubunge wa jimbo hilo Godfrey Mgimwa wakiondoka mara baada ya mazishi hayo 23Kiongozi wa Chama cha Chadema akizungumza katika mazishi hayo ambapo Chama hicho kimetoa ubani wa shilingi elfu hamsini. 24Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba akizunguza katika mazishi  hayo ambapo Chama cha Mapinduzi kilitoa ubani wa shilingi milioni moja taslimu kulia ni  mgombea ubunge wa jimbo hilo Godfrey Mgimwa 25Hili ndilo gari lililosababisha vifo vya vijana hao.

No comments:

Post a Comment