TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, March 4, 2014

SIMBA, RUVU SHOOTING MILIONI 20 TU!, KWELI MASHABIKI WAMESUSA?, WANA SIMBA WAJIPANGE UPYA!!


Mechi ya  Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa jana (Machi 2 mwaka huu) imeingiza sh. 20,610,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 4,402,492 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 3,143,898.31.
Ni ukweli usiofichika kuwa mashabiki wa Simba sc hawana imani tena na kikosi chao chini ya kocha wao,  Raia wa Croatia, Dravko Logarusic kufuatia kukumbwa na matokeo mabaya mzunguko huu wa pili.
Katika mechi sita ilizocheza mzunguko huu wa pili, Simba imefungwa mechi mbili, kutoka sare mbili na kushinda mbili.
Ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora,  uwanja wa Taifa, Ikatoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, uwanja wa Jamhuri, ikafungwa 1-0 na Mgambo JKT Dimba la CCM Mkwakwani Tanga, ikasafiri mpaka Mbeya na kutoka sare ya 1-1 na Mbeya City.
loga+clipKweli Loga ni mkali kwa wachezaji wake?
Baada ya Mbeya ikarejea Dar es salaam uwanja wa Taifa na kufungwa mabao 3-2 na JKT Ruvu, hatimaye jana ikafanikiwa kupata ushindi wa pili dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kuilaza mabao 3-2, huku mshambuliaji wake hatari, Amiss Tambwe akifikisha mabao 19 baada ya kufunga mawili jana kipindi cha kwanza.
Simba na Yanga ni klabu kongwe hapa nchini na zimejizolea mashabiki lukuki kila kona ya Tanzania na nje ya Tanzania.
???????????????????????????????Mwenyekiti wa Simba Sc, Ismail Aden Rage
Mashabiki-wa-Simba
Umati mkubwa kama huu siku hizi hautokei tena uwanjani
Imekuwa ni suala la kawaida kwa timu hizi zinaposhuka dimbani, mashabiki wake kufurika kwa wingi kuona namna vikosi vyao vinavyosakata kabumbu.
Mapato ya mlangoni yamekuwa muhimu sana kuendesha klabu za Simba,  Yanga kutokana na kuwa na mtaji wa mashabiki wengi zaidi ya klabu yoyote nchini.

No comments:

Post a Comment