TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 5, 2014

Tahadhari ya mvua kubwa/heavy rainfall warning 05-07/03/2014


radar
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA 
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz 
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 04 Machi, 2014 
Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa. 
Taarifa Na. 201403-01
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki Saa 10:00 Jioni
Daraja la Taarifa: Tahadhari
Kuanzia: Tarehe 05 Machi, 2014 
Mpaka: Tarehe 07 Machi, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24
vinatarajiwa.
Kiwango cha uhakika: Wastani (65%)
Maeneo yanayotarajiwa
kuathirika
Ukanda wote wa Pwani (Mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es
Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuimalika kwa mgandamizo mdogo wa hewa
mashariki mwa bahari ya Hindi sambamba na kusogea kwa haraka kwa
mfumo wa mvua za msimu (ITCZ) hivyo kuongeza kiwango cha
unyevunyevu kutoka baharini kuelekea maeneo tajwa hapo juu.
Angalizo:
Wakazi na watumiaji wa Bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na
maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki.
Maelezo ya Ziada
Mvua zinazoendelea na zinazotarajiwa kunyesha zinaashiria kuanza
mapema kwa mvua za masika katika baadhi ya maeneo ya pwani ya
kasikazini ikiwemo Dar es Salaam.
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa
mrejeo kila itakapobidi.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

No comments:

Post a Comment