TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 8, 2014

MASAU BWIRE AUNGURUMA NA MTANDAO

ruvu-shooting-oct1-2013Msemaji wa maafande wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametamba kuwa klabu yao imejiandaa vizuri kuwazamisha maafande wenzao kutoka kule jijini Arusha, uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani.
Shooting wameingia katika rekodi msimu huu wa 2013/2014 baada ya kufungwa mabao 7-0 na Yanga ya Dar es salaam katika dimba la Taifa.
Timu nyingine ambazo zimekula kipigo kikali ni JKT Ruvu waliofungwa mabao 6-0 na Prisons.
Mgambo JKT walifungwa 6-0 na Simba mzunguko wa kwanza, huku Ashanti nao wakila kipigo cha 5-1 kutoka kwa Yanga.

HALL AKIRI LIGI KUU MSIMU HUU NI BORA, APONDA UBABAISHAJI WA VIONGOZI SOKA LA BONGO!!

Hall 
Kocha wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Zanzibar na Azam fc, Sterwart John Hall
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
WAKATI ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa wakati wa magharibi kwa maana ya lala salama, aliyekuwa kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes na klabu ya Azam fc mpaka mwishoni mwa mzunguko wa kwanza msimu huu wa 2013/2014, Mwingereza Sterwart John Hall amesema msimu huu una ushindani mkubwa zaidi ya msimu uliopita.
Katika mahojiano maalumu na mtandao huu, Hall alisema imekuwa jambo zuri kuibuka kwa timu ngumu kama Mbeya City, lakini bado kuna timu dhaifu nyingi kitu ambacho si kizuri katika ligi.
“Nikiwa kocha wa mpira, lazima nisema ukweli, msimu huu umekuwa bora zaidi, lakini nadhani yanahitajika maboresho zaidi kwa klabu ili kupunguza udhaifu wa timu nyingi”. Alisema Hall.
Kocha huyo aliongeza kuwa imekuwa ikishangaza sana na ni jambo zuri pale timu ndogo zinapotoa changamoto kubwa  uwanjani dhidi ya timu kubwa za Simba, Yanga na Azam fc.
“Zinahitajika timu nyingi  zenye ubora kama Mbeya  City, hapo utaona ligi bora. Kuna timu za chini, hakika zimekuwa zikionesha kiwang duni sana na kuharibu utamu wa ligi”. Alisema Hall.

No comments:

Post a Comment