TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 8, 2014

ATCL yapata ndege mpya, Yaanza utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha huduma zake

ATCL 2Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL, Kapteni Milton Lazaro (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo mara baada ya kuwasili kwa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku.ATCL 3 Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la ATCL, Kapteni Milton Lazaro (Kulia) akiwatambulisha baadhi ya watendaji wa shirika hilo mara baada ya kuwasili kwa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku.ATCL 4 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Taifa Air Tanzania (ATCL) wakisheherekea mara baada ya kuwasili kwa ndege mpya ya shirika hilo aina ya CRJ-200, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku.ATCL 5 ATCL 6Picha ya ndege mpya ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL), aina ya CRJ-200 ya nchini Canada, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Alhamis usiku.
……………………………………………………………………………………………………………..
  •  Yaanza utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha huduma zake
  • Kupata ndege mbili mpya zenye uwezo wa kubeba abiria 78 ifikapo mwezi Mei
  • Yaondoa adhabu na masharti magumu kwa abiria wanaobadilisha tarehe za safari na wanaochelewa kufika uwanjani siku ya safari 
Na Mwandishi Wetu.
SHIRIKA la Ndege la Taifa (Air Tanzania) limepata ndege nyingine aina ya CRJ-200 ya nchini Canada yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wake madhubuti wa kuimarisha huduma zake.
Shirika hilo la Air Tanzania (ATCL) linaona ujio wa ndege hii kama chachu ya kutimiza azma yake ya kuimarisha huduma zake ikiwa ni pamoja na kuongeza safari zake katika njia wanazoruka kwa sasa, kuanzisha njia nyingine mpya, na kuwahakikishia wateja wake uhakika wa huduma zake.  
Mara tu baada ya ndege hiyo kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Alhamis usiku, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Captain Milton Lazaro alisema kuwa kuna matumaini makubwa ya Shirika la Ndege la Taifa kufanya vizuri zaidi katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga, ikizingatiwa kuwa shirika lina mkakati madhubuti wa upanuzi wa huduma zake ambao utekelezaji wake umeanza.
“Ndege tuliyoipokea leo hii, ni sehemu ya ndege tatu tulizopanga kuleta mwaka huu. Ndege nyingine mbili zinatarajiwa kufika kati ya mwezi Aprili na Mei mwaka huu. Kuongezeka kwa idadi ya ndege zetu kutatuwezesha sisi kufungua mipaka kwa kuanzisha njia mpya na kuongeza safari nyingi zaidi katika maeneo tunayoenda kwa sasa,” alisema Kapteni Lazaro.  
Alisema kuwa ndege mbili zitakazoletwa nchini ifikapo Mei, zinauwezo wa kubeba abiria 78 na ni toleo jipya katika sekta ya usafiri wa anga, na zitatumika katika kusafirisha abiria ndani na nje ya nchi.
Kapteni Lazaro alisema kuwa shirika lake linampango wa kuanzisha safari mpya ikiwa ni pamoja na ya Tabora – Mpanda, Mbeya- Dar es Salaam na kuongeza idadi ya safari za Mwanza- Dar es Salaam, Dar es Salaam-Comoros na Mtwara pamoja na Kigoma.
“Kwa ongezeko hili la safari zetu, abiria wetu watafurahia safari za kila siku za kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ikiwa muda wa kuondoka Dar kuwa 1600hrs na kutoka Mwanza kuwa 1800hrs. Tutakuwa tukienda mkoani Mbeya mara nne kwa wiki; kwa siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili. Wakati Moroni katika visiwa vya Comoro tutakwenda katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi. Na pia tunategemea kuzindua safari ya Tabora – Mpanda hivi karibuni,” alisema.  
Aliongeza kuwa shirika hilo pia limeondoa baadhi ya adhabu watozwazo abiria endapo wanashindwa kusafiri siku na muda waliyoomba, na kusema kuwa hii itawasaidia abiria wao kutoingia gharama za ziada endapo watakumbana na dharura mbali mbali kabla ya safari.
“Katika jitihada za kuwasaidia abiria wetu na kuwaonyesha kuwa tunayatambua mazingira tunayoishi na yakibiashara vizuri, shirika limeamua kuondoa adhabu kwa abiria ambao watashindwa kufika uwanja wa ndege kabla ya muda wa ndege kuondoka na adhabu ya kubadilisha safari,” alisema Kapteni Lazaro.
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji huyo, upatikanaji wa ndege hiyo utaongeza idadi ya abiria kwa kati ya asilimia 30 mpaka 40, kutokana na kuwa huduma za shirika hilo bado ni nzuri na viwango vya nauli ni vya kiushindani zaidi na vyenye unafuu ukilinganisha na mashirika mengine.
Kwa kutumia ndege yake aina ya Bombardier Dash-8, ATCL kwa sasa inasafiri katika zaidi ya maeneo nane (8) nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na Mtwara, Mwanza, Tabora, Kigoma, Dar es Salaam, Mbeya, Bujumbura na Moroni nchini Comoro.

No comments:

Post a Comment