TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 3, 2014

MAN CITY MABINGWA CAPITAL ONE, PELLEGRINI APUMUA!!

MANCHESTER City chini ya kocha wake, Manuel Pellegrini  imefanikiwa kutwaa Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland usiku wa jana Uwanja wa Wembely, London.
 Man City  waliuanza vibaya mchezo huo baada ya kutanguliwa na Sunderland kwa bao la Borini dakika ya 10 kabla ya kuzinduka kipindi cha pili na kuwafumua Sunderland.
Wafungaji wa mabao ya City walikuwa ni Yaya Toure dakika ya 55, Samir Nasri dakika ya 56 na Jesus Navas dakika ya 90.
Baada ya kutwaa kikombe hicho, sasa Man Pellegrini anapata la kuongea kufuatia kufanya vibaya kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Barcelona, ambapo walilala mabao 2-0 kutoka kwa wakali wa dunia, FC Barcelona na yeye kumshambulia refa na baadaye kufungiwa mechi tatu.
Lakini hakufanya vibaya pekee yake UEFA, hata, hata Arsene Wenger na David Moyes walikula vipigo vya 2-0, huku Chelsea pekee kwa klabu kutoka England ikiambulia sare ya bao 1-1 huko Uturuki.
Kikosi cha Man City kilikuwa: Pantilimon, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov, Nasri, Toure, Fernandinho, Silva/Javi Garcia dk77, Dzeko/Negredo dk88 na Aguero/Navas dk58. 
Sunderland: Mannone, Bardsley, Brown, O’Shea, Alonso, Ki, Larsson/Fletcher dk60, Cattermole/Giaccherini dk77, Colback, Johnson/Gardner dk60 na Borini.  
Mabingwa: Manchester City wametwaa taji la Capital One Cup kwa kuifunga Sunderland 3-1 kwenye fainali
Delight: Nasri converted a deflected cross from the left from Aleksandar Kolarov
 Mfaransa mwenye kipaji kikubwa, Nasri akishangilia baada ya kufunga
Scrum: Manchester City players celebrate after taking the lead at Wembley
 Wachezaji wa Manchester City wakisherehekea Uwanja wa Wembley
Mbali na mcheo huo wa Capital one, ligi kuu soka nchini England iliendelea kwa mechi tatu kupigwa.
Tottenham wakiwa nyumbani kwao walishinda bao 1-0 dhidi ya Cardif City. Bao pekee la ushindi lilifungwa na Roberto Soldado akipokea pasi kutoka kwa Emmanuel Adebayor.
Matokeo kwa ujumla yalikuwa hivi;
England: Premier League
 
 
 
Finished
 
 Tottenham
1-0
Cardiff
 
(1-0)        
 
Finished
 
 Swansea
1-1
Crystal Palace
 
(1-0)        
 
Finished
 
 Aston Villa
4-1
Norwich

No comments:

Post a Comment