TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 5, 2014

POMBE YAPIGWA MARUFUKU TWIGA STARS

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

NDOTO kubwa ya wanandinga wa Tanzania na Afrika nzima ni kucheza soka la kulipwa katika ligi kubwa duniani kama vile ligi kuu nchini England, Hispania, Ujerumani, Ufaransa, na Italia.
Hakuna mwanasoka mwenye malengo asiwaze kucheza katika ligi hizo zilizosheheni klabu zenye mvuto mkubwa zaidi duniani na wanasoka bora wa Dunia.
Hakika ni sifa kubwa sana kwa mchezaji wa Kiafrika kuonekana katika runinga akisakata kabumbu anga za kimataifa. Simaanishi anaishia kupata sifa tu, bali hata `mkwanja` unaopatikana katika soka hilo ni mkubwa.
Nani asiyefahamu utajiri wa Samuel Eto`o, Didier Drogba, Yaya Toure na wengine wengi kutoka nchi za magharibi mwa Afrika.
DSC_8979Hapa Tanzania bado hatujafanikiwa kupata wanasoka mahiri wa kwenda kucheza ligi za wenzetu zaidi ya kuwaona wachezaji wetu wakienda kucheza ligi za kawaida kabisa huko Uarabuni na mataifa ya kiwango cha chini kisoka barani Ulaya.
Wengine kama Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wamejaribu na wamethubutu na ndio maana unawasikia na kuwaona TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
TP Mazembe ni moja ya klabu kubwa yenye utajiri mkubwa barani Afrika. Kwa wachezaji wa Kitanzania ni moja ya klabu inayowafaa na ndio maana Samatta alitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.
DSC_0608Kocha Kaijage akiwa na vijana wake kwenye moja ya mazoezi ya Twiga Stars uwanja wa Karume, jijini Dar es salaam
Ukiwauliza wachezaji wengi wa Tanzania, nini malengo yao? Jibu huwa ni jepesi sana “nataka kucheza soka la kulipwa”. Sio tatizo kwa jibu hili, lakini bado ipo haja ya kujiuliza tena, huyu anayetaka kucheza soka hilo anaweza kutimiza ndoto hizo?.
Swali hili huwa linanikosesha majibu ya haraka kila nikitafakari hali halisi ya wachezaji wa Kitanzania ambapo wengi wao wana malengo makubwa, lakini utekelezaji wake ni mdogo sana, nidhamu mbovu na kulewa sifa wakati bado hajafanikiwa malengo yake.
Achana na hayo, kwasasa Dunia  inajadili sana soka la wanawake.

No comments:

Post a Comment