TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 8, 2014

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI, JOHN MINJA AHUDHURIA SHEREHE ZA KUFUNGA RASMI MAFUNZO KOZI NAMBA 08 YA MWAKA 2014 KWA MAAFISA MAGEREZA NCHINI MSUMBIJI

1 Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Emilio Guebuza(kulia vazi jeupe) akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maafisa Magereza Wahitimu wa taaluma ya Uaskari Magereza Nchini Msumbiji katika Sherehe za kufunga Mafunzo hayo zilizofanyika Machi 07, 2014 katika Chuo cha Maafisa Magereza kilichopo Maputo, Msumbiji ambapo Nchi mbalimbali za Afrika zilialikwa zikiwemo Afrika Kusini, Zambia, Namibia, Zimbabwe, Swaziland pamoja na Tanzania. Jumla ya Wahitimu Maafisa 430 wamehitimu vyema mafunzo hayo ya Uaskari wa Magereza.2 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja(wa nne toka kulia) akiwa meza Kuu pamoja na Wakuu wa Magereza toka nchi mbalimbali za Afrika katika Sherehe za kufunga rasmi Mafunzo ya taaluma ya Uaskari Magereza kwa Maafisa Magereza wa Msumbiji. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Emilio Guebuza(wa tatu toka kulia) ni Kamishna wa Magereza nchini Zambia, Percy Chato.3 Gadi ya Maafisa Magereza wa Msumbiji Wanaume wakipita kwa mwendo wa haraka wakitoa heshima mbele ya Mgeni rasmi, Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Emilio Guebuza katika hafla fupi ya ufungaji Mafunzo ya taaluma ya Uaskari Magereza kwa Maafisa 430 wa Magereza yaliyofanyika Machi 07, 2014 Maputo, Msumbiji.4Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja akisalimiana kwa kushikana mikono na Rais wa Msumbiji, Mhe. Armando Emilio Guebuza(kama wanavyoonekana katika picha) baada ya hafla fupi iliyotanguliwa na Gwaride Maalum katika Sherehe za kufunga rasmi Mafunzo ya taaluma ya Uaskari Magereza ambapo jumla ya Maafisa Magereza 430 wamehitimu taaluma hiyo Machi 07, 2014 Maputo, Msumbiji (kulia pembeni kwa Jenerali Minja) ni Waziri wa Sheria Nchini Msumbiji, Mhe. Bervinda Levi.5Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania, John Casmir Minja(wa nne toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya Urekebishaji/Magereza Afrika, Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Nchini Msumbiji pamoja Maafisa Magereza Wahitimu wa Kozi namba 08 ya Mwaka 2014 ya taaluma ya Magereza (upande wa kulia). Wa tano toka kulia ni Kamishna wa Magereza Nchini Zambia, Percy Chato(wa tano toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment