TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 5, 2014

Pinda, Mengi, Askofu Gamanywa, Mzee wa Upako wachuana Tamasha la Pasaka

DSC060441-300x200Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mizengo Pinda amechomoza kwenye zoezi la upigaji kura kuchagua mgeni rasmi katika tamasha hilo linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa Tanzania.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era sambamba na Waziri Mkuu, wengine wanaofuatia katika zoezi hilo ni Mkurugenzi wa kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi  na Askofu Mkuu wa Taasisi ya WAPO Mission International, Sylvester Gamanywa,  mchungaji wa kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat Gwajima, Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ pia wanamfuatia Waziri Mkuu katika zoezi la upigaji kura linaloendelea. Mang’era anaendelea kuwakumbusha watanzania namna ya kuwapigia kura waimbaji, mgeni rasmi na mikoa ambako ukitaka kumpigia mwimbaji andika pasaka acha nafsi kisha andika jina la mwimbaji unatuma kwenda namba 15327. Pia kwa mgeni rasmi  andika neno pasaka acha nafasi kisha andika jina la mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda 15327, wakati mikoa unaandika pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura tuma kwenda namba 15327 piga kura uwezavyo ili upate mwimbaji na mgeni rasmi na mkoa unaopenda ili tamasha lifanyike. Aidha Mang’era mbali ya viongozi hao wa dini na serikali, pia waimbaji Jescar BM  na Bahati Bukuku ni mojawapo ya waimbaji wanaoonekana kuelekea kupata nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo kwa kuwa na kura nyingi. Mang’era alisema mikoa ambayo inaongoza kupigiwa kura nyingi ni pamoja na Mwanza, Mbeya, Kigoma na Dar es Salaam inapigiwa kura nyingi kwa ajili ya kufanyika kwa tamasha hilo. Makamu Mwenyekiti huyo alisema kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo wanazingatia na kutekeleza yale ambayo yanayotakiwa na wadau ambao wanachagua wanachopenda.

No comments:

Post a Comment