TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, March 4, 2014

MNYAMA SIMBA ATISHIWA KUVUTWA SHARUBU MBEYA, `UCHAWI` WA LOGA UTAWAOKOA!!

SIMBASC2 
Vijana wa Logarusic wana kibarua kizito machi 9 jijini Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons. Na tayari wameshapigwa Mkwara mzito wa kurejea na maumivu ya kufungwa.
TFF-Tanzania-PrisonsHawa nao safari hii ni hatari tupu, wamekuja juu sana

WAJELAJELA Tanzania Prisons wametamba kuibamiza Simba Sc ya jijini Dar es salaam katika mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara jumapili ya machi 9 mwaka huu uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza kwa kujiamini na mtandao huu, katibu mkuu wa klabu hiyo Inspekta Sadick Jumbe, amesema mnyama hana ubavu wa kutoka katika mchezo huo kutokana na kuimarika kwa kikosi chao mzunguko huu wa pili wa ligi kuu.
“Lazima ufahamu kuwa kikosi chetu chini ya kocha wetu David Mwamwaja kimeimarika sana. Mpaka sasa hatujapoteza mechi hata moja. Jana Mgambo wametubana mbavu na kutoka nao sare ya 1-1, lakini nakuhakikishia, tuna hamu na mnyama jumapili na hataweza kutoka”. Alisema Jumbe.

No comments:

Post a Comment