TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 5, 2014

Mkazi wa Bukoba ashinda milioni 50 za Airtel ‘Mimi ni Bingwa’!!

1Afisa uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde(kulia)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa droo ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ iliyochezeshwa Jumanne jioni katika ofisi za makao makuu ya Airtel. Bw. Rashid Jackob Kagombola, mkazi wa Bukoba  mkoani Kagera alitangazwa mshindi wa shilingi milioni 50. Kushoto ni Mkaguzi mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Bw. Bakari Maggid.5Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde (kulia) akimwonyesha Mkaguzi mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Bw. Bakari Maggid namba ya katika droo kubwa ya promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ iliyochezeshwa Jumanne jioni katika ofisi za makao makuu ya Airtel.  Bw. Rashid Jackob Kagombola, mkazi wa Bukoba mkoani  Kagera alitangazwa mshindi wa shilingi milioni 50.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania kupitia promosheni yake ya ‘Mimi ni Bingwa’ imemfanya Bw. Rashid Jacob Kagombola, mkazi wa Bukoba mkoani Kagera kuwa tajiri baada ya kujishindia milioni 50 katika droo kubwa ya bahati nasibu iliyochezeshwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Akimtangaza mshindi Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “Leo hii tumefikia mwisho wa promosheni yetu ya ‘Mimi ni Bingwa’ ambayo imewanufaisha watanzania walio wengi. Limekuwa ni zoezi lenye mafanikio makubwa likiwa na idadi kubwa ya wateja wakijiunga katika promosheni na kujishindia zawadi katika vipengere tofauti. 
“Ningependa kuwashukuru wateja wetu kwa kushiriki katika promosheni hii tangu ilipoanza mwishoni mwa mwezi November mwaka jana. Airtel bado mipango mingine mingi inakuja, tukilenga kuendelea kurudisha kile tulichonacho kwa wateja wetu na kuisaidia jamii inayotuzunguka kukuza viwango vyao vya kuishi,” alisema Mmbando. 
Alisisitiza kuwa mbali na zawadi kubwa ya milioni 50 kutolewa, washindi wa awamu ya pili na ya tatu wa safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya moja kwa moja ‘live’ ya klabu ya Manchester United wataondoka nchini mwezi huu pale klabu hiyo ikitarajia kucheza tena katika uwanja wa Old Trafford.  
Kwa upande wake, milionea mpya akizungumza kupitia simu kutoka Bukoba aliipongeza Airtel Tanzania kwa kuanzisha promosheni zinazosaidia kuyabadilisha maisha ya wateja wake na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na nchi nzima kwa ujumla.
“Hii ni miujiza inayotokea maishani mwangu. Siwezi kuamini nami nimeingia katika orodha ya mamilionea Tanzania. Ni kama ndoto kwangu imekuwa kweli sababu ya Airtel. Naishukuru Airtel Tanzania kwa msaada wao si tu kwa wateja wake bali pia kwa jamii yote inayoizunguka. Hizi milioni 50 hakika zitabadilisha maisha yangu kabisa na zawadi nitakayoipatia Airtel ni kubaki kuwa mteja wao mwaminifu wakati wote,” alisema Bw. Kagombola.
“Nimejiunga na promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ tangu ilipoanza mwezi November, na nilikuwa nikicheza pale tu nitakapokuwa na salio la kutosha. Ilikuwa ni changamoto kuweza kupata pesa ili kuongeza salio la muda wa maongezi, lakini siwezi kuamini leo hii mimi ni milionea! Shukrani ziende kwa promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ kwa kubadilisha maisha yangu,” aliongeza. 
Promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ imeanza mwezi Novemba mwaka jana, ikiwa ni matokea ya ushirikiano katika ya klabu ya Manchester United na kampuni hiyo ya simu, haikulenga kuwazawadia wateja pekee, bali pia kuwaunganisha washiriki na soka la kimataifa na kusaidia kukuza hari ya michezo miongoni mwa watanzania.                                                             
Wakati wa promosheni hiyo, washiriki wawili wa Mimi ni Bingwa walizawadiwa shilingi milioni 2 kila siku, wawili wakijishindia shilingi milioni 5 katika droo za kila wiki na mmoja kujishindia tiketi mbili za safari iliyogharamiwa kila kitu kwenda Old Trafford.

No comments:

Post a Comment