TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 5, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207“PRESS RELEASE” TAREHE 04.03.2014. 
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MKAZI MMOJA WA JIJINI MBEYA AKIWA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI. 
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI. 
  • MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI. 
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA BIASHARA BAADA YA MUDA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MKAZI MMOJA WA JIJINI MBEYA AKIWA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA YONA MWANJELA (29) MFANYABIASHARA,    MKAZI WA NZOVWE AKIWA NA MAFUTA YA DIESEL MAPIPA MAWILI NA NUSU [2 ½] MADUMU 38 KILA DUMU LIKIWA NA UJAZO WA LITA 20 JUMLA YA MAFUTA YOTE NI UJAZO WA LITA 1,260 MALI IDHANIWAYO KUWA NI YA WIZI. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.03.2014 MAJIRA YA SAA 15:30HRS ALASIRI HUKO KATIKA ENEO LA NZOVWE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA SHUGHULI HIZI KWANI NI VITUO VYA MAFUTA NDIVYO VYENYE LESENI YA KUFANYA SHUGHULI HIZI. PIA NI HATARI KWA MAISHA YA WATU WANAOISHI MAENEO YA KARIBU PA.LE ITOKEAPO AJALI YA KULIPUKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO KWA JESHI LA POLISI JUU YA SHUGHULI WANAZOFANYA ILI WAWEZE KUFUATILIWA KWA KARIBU ZAIDI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VICTORIA SEMPONDA (50) MFANYABIASHARA, MKAZI WA MAFIATI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05]. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 03.03.2014 MAJIRA YA SAA 13:15HRS MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA MAFIATI, KATA YA MAANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI/MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI/USAMBAZAJI/UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI.
MWANAUME MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NOAH ANTHONY (26) MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILEMI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE MOJA SAWA NA UZITO WA GRAM 05. MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 03.03.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA HUKO KATIKA ENEO LA MAFIATI, KATA YA MAANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA KULIMA/KUSAMBAZA/KUUZA DAWA HIZO ZA KULEVYA AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA JIJINI MBEYA KWA KOSA LA KUFANYA BIASHARA BAADA YA MUDA.
MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FAUSTINE CHENGULA (28) MKAZI WA NZOVWE NA WENZAKE WATANO [05] WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA WANAFANYABIASHARA YA POMBE BAADA YA MUDA KUISHA. WATUHUMIWA KWA PAMOJA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 04.03.2014 MAJIRA YA SAA 01:05HRS USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA ENEO LA NZOVWE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHAMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUFUATA NA KUZINGATIA TARATIBU ZA KUENDESHA/KUFANYA BIASHARA ZAO ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment