TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, March 7, 2014

KIONGOZI UVCCM AFUNGA TAWI LA CHADEMA NA KUPANDISHA BENDERA YA CCM-LUSHOTO

IMG-20140306-WA0034 IMG-20140306-WA0035Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko amefunga tawi la Chadema katika Kijiji Cha Lukozi na kupandisha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza Ufalme mpya wa Chama hicho cha siasa.
Tukio hilo limetokea jana tarehe 6th March 2014 katika kijiji cha Lukozi, wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga, ambapo sambamba na kuasisi tawi hilo la Chama Cha Mapinduzi pia kiongozi huyo wa UVCCM ameingiza wanachama wapya 206 ambapo wengi wao walikuwa ni wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 
Mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM, alifungua mashina sita yakiwemo ya Manyara, bodaboda, n.k pia alifanya vikao vinne vya ndani ambapo alizungumza na wanaCCM juu ya hali ya Uimara wa Chama na kuhoji kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Kijiji hicho ndani ya Wilaya ya Lushoto pamoja na kufanya mkutano wa hadhara ambao ulihudhuriwa na wananchi wengi wa Lukozi.
Pamoja na vikao hivyo lakini pia Husna alitembelea vikundi vya ujasiriamali vya  akinamama pamoja na kambi ya JUDO ya Vijana wilayani Lushoto na kujadili nao Changamoto wanazokutana nao na kushirikiana nao kuzipatia ufumbuzi.
Husna anafanya ziara za kawaida katika Mkoa mzima wa Tanga katika kuhamasisha Vijana kujiunga na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Vijana.

No comments:

Post a Comment