TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 17, 2014

BODI YA UCHUNGUZI WA AJALI YA MV KILIMANJARO 2 YAKABIDHI RIPOTI YAKE KWA WAZIRI WA MIUNDOMBUNU NA MAWASILIANO ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis Ramadhan Abdallah (kushoto) akikabidhi Ripoti ya Bodi hiyo baada ya kukamilika kwa Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
DSC_1303Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis Ramadhan Abdallah (katikati) akisoma baadhi ya vipengele vya Ripoti hiyo wakati wa kumkabidhi  Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar Rashid Seif Suleiman (Mwenye Kanzu)Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Picha na Nafisa M. Ali-WMM
………………………………………..
Na Nafisa M. Ali –WMM          17/03/2014
Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 leo imekabidhi rasmi Ripoti ya ajali hiyo baada ya kumaliza kazi hiyo kwa Waziri wa  Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akikabidhi Ripoti hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Khamis Ramadhan Abdallah amesema kazi hiyo waliyopewa wameweza kuimaliza kwa mujibu wa siku walizopewa na walikuwa huru bila ya kuingiliwa na mkono wa Serikali wala Taasisi yoyote.
Aidha alisema Bodi ilifanya kazi katika mazingira magumu lakini walichukulia kazi hiyo niyanyumbani na niwajibu wao kufanya kwa Maslahi ya wananchi wa Zanzibar.
Hata hivyo alisema hapo awali kazi hiyo walipangiwa kuifanya kwa kipindi cha mwezi mmoja lakini kutokana na uzito wa kazi hiyo na majukumu mengine walilazimika kuomba mwezi mmoja ambapo kazi hiyo walitakiwa kuikabidhi kesho na badala yake wameweza kuikabidhi jana.
Aidha mwenyekiti huyo alitoa shukran zake za dhati kwa niaba ya bodi hiyo kwa mamlaka ya Usafiri Baharini kwa ushirikiano mzuri waliouonesha kwa bodi hiyo kwa kipindi chote cha kazi hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman ameipongeza Bodi hiyo kwa kufanya kazi bila ya upendeleo na zaidi walizingatia uhalisia wa kazi yao na siyo kubabaishwa na Mtu.
Aidha alisema chombo hicho hakikuundwa kwa kutafutwa nani mbaya wala mkosa wa ajali hiyo bali kimeundwa kwa ajili ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuweza kurekebishwa ili Wazanzibari wasizidi kuumia.
Hata hivyo alisema dalili nzuri ipo katika Ripoti hiyo na kazi iliyobaki ni kuisoma kwa kina na kisha kukabidhi katika Mikono ya Serikali kuu kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
Aidha aliishukuru sana bodi hiyo kwa vile ilikuwa huru na kuweza kufanya kazi kwa kina bila kizuizi cha mtu wala Serikali.
Naye Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Tahir A.K Abdullah amesema Wananchi hivi sasa wanasubiri kuona Serikali imefanya nini tokea ajali hiyo imetokea ambapo aliwatoa wasiwasi kuwa haki  itatendeka kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika.
Bodi hiyo ya Wajumbe watano ambayo iliyoundwa chini ya Sheria ya Usafiri wa Baharini kifungu no. 4552 na 4551 ya mwaka 2006 imeundwa kufuatia ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 iliyotokea Miezi miwili iliyopita katika Mkondo wa Nungwi ilipokuwa ikitokea Pemba kuja Unguja.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment