TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, March 21, 2014

MWIGULU ATAKA MAJESHI YA TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MAJESHI YA NCHI NYINGINE

MWIGULUNCHEMBA 
NAIBU waziri wa fedha,Mwigulu Nchemba amesema, kukua kwa utandawazi kumeifanya dunia kuwa  kijiji , hivyo kuna kila hali ya kuimarisha majeshi ya ulinzi  ya ndani kwa kushirikiana na majeshi ya nchi za nje kwa kuyaongezea ujuzi zaidi wa kinadhalia katika kuimarisha usalama wa nchi.
Kauli hiyo ameitoa jana katika mahafari ya kwanza ya kuhitimu kozi ya mafunzo mkakati kwa maafisa wa jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ)kutoka chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli(TMA) baada ya kumaliza kozi  ya mwaka mmoja katika chuo cha uhasibu Njiro(IAA),ambapo jumla ya maofisa  52 kutoka nchi 10 za Afrika  wahitimu kozi ya shahada ya udhamili na stashahada na kutunukiwa vyeti .
Nchemba alisema kuwa kwa sasa nchi nyingi za afrika haziitaji kupigana kwa ajili ya kupata uhuru ila zinahitaji ulinzi ili kupiga hatua katika masuala ya kiuchumi wakati nchi hizo zikiwa salama ,hivyo alitoa rai kwa mafunzo hayo kuendelezwa zaidi katika  program mbalimbali ambazo zitasaidia wahitimu kufanya vizuri zaidi katika kuimarisha utendaji wa kazi zao.
Alisisitiza kuwa lazima majeshi ya kiafrika yajiendeshe kisasa zaidi kwa kutumia elimu na ujuzi kutoka kwenye vyuo mbalimbali vya ndani na nje ili kwendana na hali ya utandawazi na teknolojia ya kisasa.
Naye mkuu wa chuo hicho Prof,Johannes Monyo alisema kuwa ushirikiano wa chuo cha uhasibu Arusha na chuo cha kijeshi Monduli ulikuja kwa kutiliana saini mapema mwaka jana,katika kutoa taaluma hiyo baada ya mitaala yake kupitishwa na taasisi ya elimu ya juu(Nacte).
Alisema mafunzo hayo yatawasaidia wanajeshi hao na raia  kuongeza ujuzi katika shughuli zao,na kwamba chuo hicho kinatarajia  kuanzisha program nyingine ya mafunzo inayotarajiwa kuanza mapema mwakani,baada ya mtaala yake kukamilisha na kupitishwa.
Monyo alisema makubalinao ya kuanzisha mafunzo hayo yanawezesha chuo hicho kupeana mafunzo juu ya kuboresha masuala mbalimbali ya kitaaluma ikiwemo katika sekta ya fedha,utawala na diplomasia.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaida pia kuwapa  ujuzi wa kimkakati  katika masuala ya Kiuongozi ,kutatua migogoro,usimamizi wa miradi,Diplomasia,Mawasiliano na sekta za kiraia, na matumizi ya teknolojia  .
Alisema chuo hicho kilianza kutoa kozi ya kwanza kwa maofisa wa jeshi zaidi ya 52 pamoja na wakufunzi kutoka TMA wanaotoka katika Nchi mbalimbali zikiwemo za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na Nchi za Kusini mwa Jangwa la Afrika (SADC) .

No comments:

Post a Comment