TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, March 21, 2014

MSD, CSR WAJITOLEA KUMSAFIRISHA MTOTO ALIYEUNGUA MOTO KUTOKA MBEYA KWENDA HOSPITALI YA CCBRT DAR ES SALAAM KWA MATIBABU

1 
Mama wa mtoto Dorothea Njavike (1) ambaye aliunga moto mkoani akiwa mchanga na kuathirika kwa kupata ulemavu, Milka Kabelege (kulia), mama mkubwa wa mtoto huyo, Salome Kyegulo (kushoto), wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam juzi ambapo wamefika jiji kupata matibabu katika Hospitali Maalumu ya CCBRT. Gharama za kusafiri kutoka mkoani Mbeya kwa ndege kuja Dar es Salaam zimefanywa na Bohari ya Dawa (MSD). (PICHA KWA HISANI YA MSD)
…………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD), imejitolea kumsafirisha hadi Dar es Salaam kwa matibabu katika Hospitali ya CCBR mtoto Dorothea Njavike (1) aliyepatwa na janga la kuungua moto mkoani akiwa mchanga.
MSD na CSR wamejitolea kummsafirisha mtoto huyo juzi pamoja na mama yake mzazi Milka Kabelege, mama yake mkubwa Salome Kyegulo kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo wakati wa matibabu yake katika hospitali hiyo maalumu ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam.
“Baada ya kupata taarifa ya kuungua mtoto huyo kupitia vyombo vya habari sisi MSD tuliguswa tukaona ni vizuri tumsaidie kumsafirisha mtoto huyo kwa ndege pamoja na wazazi wake kuja Dar es Salaam kwa kupata matibabu na kuwarudisha mkoani Mbeya baada ya matibabu” alisema Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Elangwa.
Dorothea, ambaye ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na janga la moto amepata ulemavu sehemu za uso, ambapo pua, mdomo, kidevu na jicho moja viliungua pamoja na mikono yake yote miwili kuanzia sehemu za maungio ya viganja.
Kutokana na hali hiyo juhudi mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa na vikundi mbalimbali hadi kufikia uamuzi wa kumpeleka jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Kwa mujibu wa mmoja wa wawezeshaji kutoka kundi la Motherhood la Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina moja la Anitha alisema madaktari watakao mtibu mtoto huyo ni kutoka Tanzania ambao wataungana na wale wa mataifa mengine kwa ajili ya kuangalia namna ya kuweza kurekebisha uso na maeneo mengine yaliyoathiriwa na moto huo.
Mmoja wa madaktati aliyempokea mtoto huyo juzi baada ya kufika katika Hospitali ya CCBRT ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema mtoto huyo ataanza kupata matibabu kwa hatua za awali wakati zikisubiriwa taarifa zaidi zilizomo kwenye faili lake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya akikokuwa akipatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment