TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, March 22, 2014

SERIKALI KUTOA RUZUKU KWA WAVUVI ILI KUIMARISHA SEKTA YA UVUVI NCHINI

1Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na baadhi ya waandishi wa habari wakipanda kwenye boti ndogo kwa ajili ya kuelekea kwenye kisiwa cha Bongoye kufanya mkutano. 2
Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa wamefika kwenye kisiwa cha Bongoye. 3Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na baadhi ya waandishi wa habari, wakielekea kwenye sehemu ya kufanyia mkutano. 4Msemaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dk. Mohammed Bahari akizungumza na waandishi wa habari juu ya ruzuku kwa wavuvi.Katikati ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi na mwisho ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, Baraka Mngulwi. 5Meneja Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Milali Machumu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).Katikati ni Msemaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dk. Mohammed Bahari na mwisho ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi. 6Mkurugenzi Msaidizi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, Baraka Mngulwi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ruzuku kwa wavuvi.Katikati ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Mvungi na mwisho ni Msemaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dk. Mohammed Bahari. 7Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mohammed Bahari akizungumza na waandishi wa habari juu ya ruzuku kwa wavuvi. 9Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na waandishi wa habari, wakiteremka kutoka kwenye Boti baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Sea Cliff wakitokea kisiwa cha Bongoye ambako ndiko kulikofanyika mkutano na waandishi wa habari. Picha zote na Hussein Makame
………………………………………………………………………….
Frank Mvungi- Maelezo
SERIKALI imetenga Shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili ya ruzuku kwa wavuvi katika kipindi cha mwaka wa Fedha 2013/14 ili kusaidia kukuza sekta ya uvuvi hapa nchini
Hayo yamesemwa na  Msemaji wa Wizara  ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Mohammed Bahari wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Dkt Bahari amesema kuwa ruzuku hiyo itatolewa kwa kuzingatia vigezo ikiwemo waombaji kuwa na vyama vya ushirika na vilivyosajiliwa kisheria.
Alitaja vigezo vingine kuwa ni chama cha ushirika kiwe kinafanya kazi za uvuvi kufuatana na sheria ya uvuvi na 22 ya mwaka 2003 na kanuni za uvuvi za mwaka 2009 na miongozo mbalimbali.
Aliongeza kuwa chama hicho kiwe na akaunti benki  iliyo hai na kithibitishe kuwa na uwezo wa kuchangia asilimia 40% ya gharama ya mradi husika, ambapo Serikali itachangia asilimia 60% ya gharama ya mradi husika.
“Chama husika kitapitisha maombi yao kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika kwa ajili ya kupitia maombi hayo na kuona kama yanakidhi vigezo viliwekwa na baada ya hapo kuwasilishwa Wizarani” alisema Dk. Bahari.
Alisema miradi itakayofadhiliwa ni pamoja na ununuzi wa boti za uvuvi, injini  na vifaa vingine vitakavyowawezesha wavuvi kuongeza tija katika shughuli za uvuvi
Dkt Bahari alifafanua kuwa ruzuku hiyo kwa wavuvi itakuwa na manufaa makubwa kama vile kuongeza mapato ya wavuvi na wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi.
Aliongeza kuwa ruzuku hiyo pia itaongezeka maduhuli ya Serikali, kupunguza vitendo vya uvuvi haramu,kuimarika kwa biashara ya mazao ya uvuvi na kuongeza ajira katika sekta ya uvuvi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, Baraka Mngulwi alitoa wito kwa wale wote wanajihusisha na vitendo vya uvuvi haramu kuacha tabia hiyo mara moja kwa kuwa Serikali imeimarisha doria katika maeneo yote .
Aliongeza kuwa kwa wale wanatumia nyavu  ambazo zimepigwa marufuku nao waache mara mara moja tabia hiyo na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaokwenda kinyume cha sheria ya uvuvi na. 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009.
Alizihimiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa sheria za uvuvi na kanuni zake zinazingatiwa kikamilifu na kuwa uvuvi haramu na biashara ya samaki wachanga vinadhibitiwa katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment