TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, March 20, 2014

CCM YASEMA UCHAGUZI WA KALENGA NI HAKI BIN HAKI.


  Katibu mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa,Ndugu Hassani Mtenga akizungumza na wanahabari wa Iringa katika ofisi za chama hicho mapema leo.

 Katibu mkuu wa CCM Mkoa wa Iringa,Ndugu Hassani Mtenga akizungumza na wanahabari wa Iringa katika ofisi za chama hicho mapema leo.
Sahihi halali ya Mwigulu Nchemba ambayo iko tofauti ya waraka uliosambazwa.
=======  ======  ========
Na Denis Mlowe,Iringa

KATIBU wa CCM Mkoa wa Iringa Hassani Mtenga amekanusha chama hicho kuhusishwa na waraka aliodai umesambazwa na Chadema ukihusu mchanganuo wa matumizi ya Sh Milioni 560 katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga.

Alisema propaganda za kisiasa za wapinzani ndio chanzo cha waraka huo kusambaa na kuwaonyesha waandishi wa habari sahihi kamili ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM  Mwigulu Nchemba anayesemekana alisaini waraka huo.

"Kwanza kuna kosa hawa wenzetu wanafanya, waraka huo una anwani ya Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa lakini chini unaonekana umesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba, sahihi ambayo imegushiwa,” alisema Mtenga
Katika waraka huo wenye kichwa cha habari kinachosema ‘Malipo ya kamati mbalimbali kwenye ushindi wa jimbo la Kalenga, umeidhinisha fedha hizo zitolewe kwa viongozi mbalimbali kama walivyoomba oili zitumike katika kampeni za jimbo.


Waraka huo unaonyesha kuwa CCM wametumia kiasi cha shilingi milioni 560 kwa ajili ya timu ya ushindi wiki hii ya mwisho ya kampeni, fedha hizo zimetumwa kutokana na tathimini yenu kuwa ni hali mbaya kwetu kwa barua yenu yenye  kumb Namba  CCM/IR/VOL11/096.
“Hakikisha kiwango hiki kinwafikia  walengwa wote wafuatao kwa uwiao tuliokubaliana kulingana na maeneo yao na wao wazigawe kwa mabalozi wetu kwenye kila kitongoji na kata apewe Balozi Sh850,000, Mama Galinoma Sh Milioni 80, Mama Ray (Ulanda) Sh Milioni 60, wenyeviti wa kata wa CCM kila mmoja Sh Milioni 20, makatibu wa kata kila mmoja Sh Milioni 8, makatibu wenezi CCM kila mmoja Sh Milioni 14 na Kamati ya ushindi Nzihi Sh Milioni 108,” sehemu ya waraka huo inasema.

Mtenga alisema lengo la kusambazwa kwa waraka huo lilikuwa kuwaaminisha wapiga kura wa Kalenga kwamba kuna fedha zimetolewa na CCM kwa ajili yao lakini zimeliwa na watu wanaotajwa katika waraka huo.
Alisema kuna kila dalili kwamba waraka huo uliandaliwa na Chadema kwa lengo la kuwarubuni wananchi wa jimbo la Kalenga wakose imani na CCM.
Wakati huo huo CCM kimempa siku 7 Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Iringa, OCD Sifael Pyuza kuwataka radhi kwa madai ya kuwadhalilisha katika ofisi za chama hicho mkoani hapa baada ya kuwafanyia uchunguzi bila kuwa na kibali maalum.

Kamanda Pyuza anatuhumiwa na chama hicho kukihusisha na mchezo mchafu wa siasa kwa kuficha watu ndani ya jengo la ofisi yake waliokuja katika uchaguzi mdogo wa Kalenga uliofanyika machi 16 na ccm kuibuka kidedea.

Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliyasema  hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuwa , Machi 16 mwaka huu kamanda huyo alituma makechero wa jeshi hilo katika ofisi za CCM za mkoa wa Iringa waliotumia mabavu kupekua ofisi moja baada ya nyingine bila kuwa na kibali halali.
Alimtaka kamanda huyo kuwaomba radhi baada ya tuhuma yake dhidi yao kubainika haina ukweli.
na chama cha mapinduzi hakiwezi kukaa kimya kwa udhalilishaji huu uliofanywa na mkuu wa upelelezi wa wilaya kwa sababu jambo hilo ni sawa na kukiingiza chama cha mapinduzi katika kashfa ya mchezo mchafu wa kisiasa.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema hana taarifa yoyote kuhusiana na madai ya chama hicho lakini yupo tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi.

No comments:

Post a Comment