TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 19, 2014

ZANTEL YAPIGA JEKI MCHEZO WA NETIBOLI!!

Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Serikali kutoka Zantel Bw. Charles Jutta akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia Mashindano ya Netiboli ya Afrika Mashariki na Kati leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga.ZT 2Kutoka kushoto ni : Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Serikali kutoka Zantel Bw. Charles Jutta, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na Katibu Mtendaji wa Chama cha Netiboli Tanzania Bi. Anna Kibira wakiwa wameshika hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 ambazo zimetolewa kama msaada na kampuni ya Zantel ili kusaidia Chaneta leo jijini Dar es Salaam.ZT 3Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 iliyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kwa ajili ya kusaidia uendeshaji mashindano ya Netiboli Afrika Mashariki na Kati leo jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………….
Na Frank Shija – WHVUM
Serikali yapokea msaada wa shilingi milioni 10 kutoka Zantel kwa lengola kusaidia Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta)leo jijini Dar es
 Salaam. Msaada huo umetolewa ili kusaidia katika mashindano ya Netiboli ya Afrika Mashariki na Kati.
Akizungumza wakati wa makabidhiano wa msaada huu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Sihaba Nkinga ameishukuru kampuni ya  Zantel kwa kuonyesha utayari wa kusaidia na kuendeleza vipaji mbambali katika Nyanja ya michezo.
“Ninaipongeza kampuni ya Zantel kwa kuonyesha utayari wake katika kusaidia kukuza vipaji vya michezo hasa katika michezo ya Netiboli, Judo na Ngumi, naamini huu ni mwanzo tu.” Alisema Bi. Sihaba Nkinga
Aidha Katibu Mkuu huyo amewaomba viongozi wa Chaneta kutumia vizuri msaada huo katika kutekeleza malengo yaliyokusudiwa ili kujenga imani
kwa wadau mbambali kuendelea kusaidia sekta ya michezo
Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Serikali kutoka Zantel Bw. Charles Jutta amesema kuwa kampuni yake imeshawishika kutoa msaada huo baada ya kuridhika na utendaji na muundo wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta)
Aliongeza kuwa msaada huu ni mwanzo wa Zantel kusaidi sekta ya michezo na kwa kuanzia wamechagua kusaidia michezo ya Netiboli, Judo na Ngumi
na ndiyo maana leo (jana) wanatoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia mashindano ya netiboli  Afrika Mashariki na Kati.
Hata hivyo Jutta amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia ukuzaji vipaji katika michezo mbalimbali na kusema kuwa ikiachiwa
Serikali peke yake haitaweza kufanikisha azma hii njema ya kufikia mafanikio katika michezo.
Wakati huo huo Katibu Mtendaji wa Chaneta Bi. Anna Kibira ameishukuru kampuni ya Zantel kwa msaada huo na kusema kuwa msaada huo umekuja
wakati muafaka ambapo chama chake kimeaanda mashindano ya kimaataifa.
Kibira aliongeza kuwa watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha msaada huo unazaa matunda na kuleta sifa kwa taifa kwa kufanikisha mashindano hayo kuwa bora na yenye kukidhi viwango vya kimataifa.
Mashindano ya mpira wa Netiboli ya Afrika Mashariki na Kati yatafanyika kuanzia tarehe 22 mwezi huu(machi)ambapo jumla timu 22
zinatarjiwa kushiriki, kati ya timu hizo timu 10 zinaumdwa na wanaume.

No comments:

Post a Comment