TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 17, 2014

ISRAEL YAPATA USHIRIKIANO NA TANZANIA KUENDELEZA KILIMO CHA BIASHARA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Picha na OMR
…………………………………….
Na Frank Shija – WHVUM
Imeelezwa kuwa Tanzania ni nchi ambayo ina ardhi kubwa na yenye rutuba amaboya haijatumiwa kwa shughuli za kilimo na uzalishaji.
Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Gharib Bilal wakati akifungua kongamano la Kibiashara Baina ya Tanzania na Israel lililoanza leo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Bilal amesema kuwa Tanzania ina jumla ya hekta milioni 44 ambazo ni nzuri na zenyerutuba na kuongeza kuwa kati ya hizo jumla ya hekta milioni 29 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
“Ndugu mwenyekiti katika hekta milioni 44 zilizopo, zaidi ya hekta  milioni 29 zinafaa kwa matumizi ya kilimo cha umwagiliaji,hivyo ni fursa kwa wawekezaji kutoka Israel kushirikiana na wananchi wa Tanzania ili kuendeleza kilimo cha kibiashara hapa nchini” Alisema Dkt. Bilal.
Aidha Dkt Bilal ameipongeza Kampuni ya Kingdom Leadership Network Tanzania ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hilo na kuongeza kuwa kupitia kongamano hilo fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo itazidi kuimarika na kukuza sekta ya kilimo ikiwemo uzalishaji wa chakula cha ziada.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) Ibrahim Kaduma ametoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa na kujishughulisha na kilimo cha kibiashara kwani ndiyo sekta pekee unayoweza ukajiari kwa faida ya uhakika.
Kaduma aliongeza kuwa kongamano ili lemelenga kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Israel hususani katika sekta ya kilimo ili kuongeza tija na kwa taifa la Tanzania.
Wakati huo huo baadhi ya washiriki wa kongamano hilo akiwemo Mkuu wa Maendeleo ya Biashara na Uhusiano wa kampuni ya Balton Tanzania Bi. Linda Byaba amesema kuwa wao wao katika kongamano ili umekuja wakati muufaka ambapo wamezindua mpango wa kufundisha vijana juu ya kilimo cha kibiashara unaojulikana kwa jina la “Farming is Cool Project”
Linda amesema kuwa kupitia mpango huo vijana wengi watanufaika kwa kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo kilimocha kisasa, elimu ya ujasiriamali na stadi za maisha na kuongeza wamekuwa na ushirikiano mzuri na Serikali hivyo mpango huu utatekelezwa kwa ufanisi na kuleta tija kwa taifa.
“Kampuni yetu imezindua mpango ambao utawanufaisha vijana wengi wa Kitanzania katika kuwapati elimu ya ujasiriamali, kilimo na stadi za maisha, hivyo napenda kutoa wito kwa vijana kutumia fursa hii kupata elimu tena inatolewa bure kabisa” Alisema Linda.
Kongamano hilo linafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere ambapo utadumu kwa muda wa siku tatu hadi alhamisi, ambapo kongamano hilo limeratibiwa na kampuni ya Kingdom Leadership Network Tanzania(KLNT) likiwa na lengo la kukutanisha wafanyabiashara wa Israel na Tanzania wanaojihusisha na sekta ya kilimo.

No comments:

Post a Comment