TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 17, 2014

MAGADI SODA KULIINGIZIA TAIFA SHILINGI BILIONI 480 KWA MWAKA

Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Katikati ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga, na Mwisho ni Afisa Habari wa Idara ya habari Frank Mvungi 
2 (6)Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba akifanunua kwa waandishi umuhimu wa mradi wa uchimbaji magadi soda  katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Kushoto ni Mhandisi wa mradi Godfrey Mahundi na Kulia ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga  
3 (6)Mhandisi wa mradi wa  magadi soda  Godfrey Mahundi akitoa ufafanuzi kuhusu makadirio ya gharama za mradi huo ambao unakadiriwa kutumia  kiasi cha dola za kimarekani milioni 500. Katikati ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Abel Ngapemba na wa mwisho ni mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Muhandisi Abdallah Mandwanga 
PICHA ZOTE  NA. Georgina Misama-MAELEZO
……………………………………………………………………..
Frank Mvungi-MAELEZO
IMEELEZWA kuwa Tanzania ni miongoni  mwa wazalishaji wakubwa wa magadi soda yatakayoingizia taifa Shilingi Bilioni  480 kwa mwaka.
Hayo yamesemwa na  Meneja Uhusiano na Mawsiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Abel Ngapemba akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Ngapemba alisema hatua hiyo inatokana na kugunduliwa kwa kwa kiasi kikubwa cha madini hayo katika Bonde la Engaruka  Wilayani Monduli mkoani Arusha.
Alizitaja faida za kugundulika kwa madini ya magadi soda kuwa ni ajira zaidi ya 500 na fedha za kigeni kutokana  na mauzo ya madini hayo nje ya nchi.
Alisema kuwa viwanda vinavyotegemea magadi soda kama malighafi ya uzalishaji hali itakayochochea kukua kwa sekta ya viwanda hapa nchini.
Ngapemba  alibainisha kuwa madini ya magadi soda yanatumika viwandani  katika utengenezaji wa bidhaa kama vioo, sabuni, dawa za meno, dawa za hosipitali, uoakaji mikate, kutengeneza  karatasi, nguo, na usafishaji wa maji.
Alifafanua kuwa utafiti uliofanywa na wataalamu wazalendo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 na ulifanyika kwa awamu  tatu yakwanza ikiwa ni uchunguzi wa awali na kutafuta maeneo ya kufanyia uchorongaji ili kubaini wingi na ubora wa magadi soda.
Alisema kuwa kazi iliyofanywa na kampuni ya OC, ambapo awamu iliyofuata ni kuangalia njia ya uvunaji wa magadi soda hayo iliyofanywa na JSC Service.
“Matokeo ya utafiti huo yameonyesha kuwapo kwa magadi soda kiasi cha mita za ujazo bilioni 4.7 na inakadiriwa kila mwaka wastani wa mita za ujazo milioni 1.9 zinaongezeka katika eneo hilo”, alisema Ngapemba na kuongeza:
Alisema kuwa NDC itahakikisha kuwa katika utekelezaji wa miradi hii mazingira hayataathiriwa na tunu za taifa zitalindwa ambapo mtazamo wa shirika hilo ni kuwapo kwa mradi wa uvunaji magadi, utalii, na ufugaji.

No comments:

Post a Comment