TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 19, 2014

MWAMBUSI SAFARINI KUMFUATA MINZIRO JUMAMOSI CHAMAZI, RICHARD PETER KUKOSA MTANANGE HUO!!

 Na Baraka Mpenja 
KIKOSI cha wagonga nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City kimeondoka leo asubuhi jijini Mbeya kuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kujiandaa mapema na mchezo wake dhidi ya Ruvu JKT machi 22 mwaka huu  uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa klabu hiyo, Freddy Jackson  wachezaji wote wapo katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo isipokuwa mchezaji Richard Peter ambaye ataukosa mchezo kwasababau hali yake haijatengamaa baada ya kuumia katika mechi yao dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora uwanja wa sokoine siku za karibuni.
Imeelezwa kuwa Peter bado  ana maumivu ya kawaida katika mbavu zake.
“Maandalizi yetu ni mazuri sana. Tumejiandaa kikamilifu,  tupo kamili kuzinyakua pointi tatu. Nayasema haya kutoka kwa kocha Juma Mwambusi”.
“Kocha anasema kikosi chake kina uwezo mkubwa sana wa kuibuka na ushindi katika mchezo huo”. Alisema Jackson katika taarifa yake asubuhi hii.
 Kwa niaba ya club, Jackson  aliweka wazi  kuwa watakuwa makini sana na mchezo huu maana wamekuwa wakioneshwa michezo mibaya sana , hasa kwa hizi timu za majeshi wanapokutana nazo.

No comments:

Post a Comment