TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, October 29, 2014

AJALI YA BODABODA NA GARI YAUA MBEYA

Mwendesha pikipiki mmoja aliyetambulika kwa jina la Vava Zakaria, anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 50 -55 aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili T.439 BDV aina ya King Lion alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari isiyofahamika namba zake za usajili wala dereva wake.
Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 08:00 mchana huko maeneo ya Tazara, kata ya Iyunga, tarafa ya Iyunga, jiji na mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya/Tuduma. 
Chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa na jeshi la polisi mkoa wa Mbeya. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Dereva alikimbia mara baada ya tukio hilo na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa vyombo vya moto kuwa makini wanapotumia vyombo hivyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika.
Aidha anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa [dereva] kuzitoa katika mamlaka husika ili akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

No comments:

Post a Comment