TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, November 1, 2014

CCM YAVUNA MAVUNO YAKE KUTOKA CHADEMA NGORONGORO

imagesNa Gladness Mushi, Ngorongoro

CHAMA cha Mapinduzi, CCM, kimezidi kujiimarisha baada ya kukisambaratisha Chama cha Chadema wilayani Ngorongoro, kufuatia hatua ya mwenyekiti wake ,Revocatus Parapara,na viongozi wa kata na matawi kubwaga manyanga na kujiunga CCM.
Tukio hilo limetokea jana kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi, uliokuwa ukihutubiwa na Katibu wa CCM, mkoa, Alphonce Kinamhala,aliyekuwa kwenye ziara ya kujitambulisha kwa wananchi uliofanyika  kijiji cha Waso wilayani Ngorongoro, na viongozi hao kujiunga rasmi na Chama cha mapinduzi.

Akihutubia mkutano huo , Katibu wa CCM, Kinamhala, amewataka madiwani wasijiingize kwenye uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa na badala yake wawaache wananchi wachague viongozi wawatakao .
Amewataka madiwani  kutokujiingiza kwenye Zabuni mbalimbali za serikali kazi zao ni kusimamia wakandarasi  ili kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa kwenye vijiji na kata inatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa. Amesema  hasara ni kubwa iwapo wao watajiingiza kwenye Zabuni watashindwa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo na mradi usipotekelezwa kwa kiwango na muda wake serikali na Chamna cha mapinduzi ndio watakaonyoshewa vidole na kulaumiwa na wao watashindwa kutetea na huko ni kukiuka majukumu yao.

 .Kuhusu mchakato wa KATIBA, Katibu Kinamhala, amewaambia wananchi wasikubali kudanganywa kwamba mchakato huo uliporwa na CCM, Katiba hiyo sio ya Chama cha Mapinduzi, bali ni ya wananchi na ndio maana imepitishwa kwenye bunge la katiba maalum, Na CCM, haijawa
Awali katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, CCM, mkoa wa Arusha, Joseph Izack  ,amewataka wanaotaka kuvuruga  amani ya nchi hii kwa kisingizio cha siasa kuacha mara moja  vinginevyo watashughulikiwa kokote pale walipo.

Ameongeza kuwa  katiba inatoa fursa kwa wanawake kugombea uongozi ngazi mbalimbali ambapo sasa wanayo nafasi ya 50 kwa 50 kila nafasi ya uongozi na haya ni mafanikio makubwa .

No comments:

Post a Comment